Tuesday, November 13, 2007

Wikendi yenu na maswala ya Somalia

Habari za leo?

Kwanza kabisa napenda kusema tena kwamba nafurahishwa na maendeleo yenu katika matumizi ya lugha. Aidha, nimeweza kujua mengi mliyoyafanya wikendi iliyopita. Je, Daudi wewe hupenda kucheza ngoma pia? Jason, kwa kawaida kila mwaka wanafunzi wangapi wapya hujiunga na timu yenu kali ya uogeleaji? Hongera sana kwa kuboresha wakati wako katika uogeleaji.

Kuhusu, Somalia mimi naamini kwamba hakuna marefu yasiyokuwa na mwisho. Kwa sababu hiyo, ipo siku Somalia itajua maana ya amani. Hata hivyo, nadhani kuwa jamii ya kimataifa yapaswa kuwasikiliza watu was nchi hiyo, na nyingine nyingi zilizo vitani, kabla ya kuyafkikia maamuzi katika hoteli mbalimbali mikutanoni. Kwa kufanya hivyo na kwa kushirikiana nadhani kuwa ufumbuzi wa matatizo yanayoikabili utawezekana.

Nawatakia safari njema ha[po kesho na mpatapo nafasi andikeni kuhusu mashindano yenu-hata kama ni kwa muhtasari tu.

Tuesday, October 30, 2007

Kumkaribisha Emily na kujitambulisha

Karibu sana Emily katika mawasiliano yetu haya. Ni furaha yetu kuwa nawe katika blogu ya Kiswahili. Aidha, asante kwa kujitambulisha kwetu. Naamini kwamba washiriki wengine nao watajitambulisha ili ujue unawasiliana na nani (mimi naamini wote mwanijua).

Hongera kwa uchaguzi wenye amani na utulivu. Je, waweza kusema machache kuhusu serekali ya wanafunzi hapo chuoni? Kwa mfano, inajumuisha viongozi wangapi na majukumu yao ya kimsingi ni nini? Wanayatekeleza vizuri? Siasa za ukabila zinajitokeza ndani yake au la? Hatimaye kwa nini wewe hukugombea nafasi yoyote? Baadaye, tutatarajia wanafuzni wa hapa Stanford kutueleza kama kuna mfumo kama huo huku.

Usiku mwema.

Sunday, October 21, 2007

Wikendi

Wikendi hii, nimeshughulika sana kwa sababu nimehitaji kufanya kazi zangu za chuo na vile vile timu yetu ya uogeleaji imekuwa na kurutu katika wikendi yote. Aidha, tulikuwa na mazoezi ya uogelaji jumamosi asubuhi na yalifuatwa na finali ya kombe cha dunia cha ragbi ambacho Afrika Kusini ilishinda.
Kwahivyo, jumamosi baada ya mazoezi, chamshakinywa na mchezo wa ragbi, nilienda kucheza 'frisbee' pamoja na timu na kurutu. 'Frisbee' ni mchezo ambao watu wanatupana diski inayoweza kuruka mbali sana. Baada ya mchezo huu, sisi wote tulienda nje kula katika mkahawa wa Meksiko. Baada ya chajio, tena pamoja tukaenda kucheza mchezo mwingine amabo katika kiingereza unaitwa 'bowling.' Katika mchezo huu, unahitaji kutupa mpira mgumu ili uangushe mingi ya miti kumi unayoweza.
Lakini, usiku wa jumamosi, baada ya kucheza 'bowling,' nilianza kuhisi vibaya, kwa hivyo niliamua kulala mapema wengine walipokuwa wakisherekea.
Sasa, asubuhi ya jumapili, ninahisi bora kuliko jana usiku lakini nina kazi nyingi ya kuandika kabla ya mwisho wa wikendi.

Tuesday, June 19, 2007

Likizo yangu ya Kiangazi 2007

19/06/07

Leo ni leo. Niliamka kwenda kuogelea mapema na nilifanya vizuri sana licha ya mwili wangu ambao umekamatwa na mafua. Baada ya mazoezi, nilirudi chumba changu kulala kidogo lakini usingizi wangu ulikuwa mkubwa kwa hivyo nilikaa kitandani kwa masaa manne! Hatimaye nilipoamka, niliandaa chakula cha mchana na nilikikula na rafiki yangu. Sasa ninaketi kwa kompyuta nikifanya mazoezi ya hii lugha safi na ninasikitika darasa letu la mwaka uliopita. Tafadhali muandike vitu vichache kueleza safari zenu!

Monday, May 14, 2007

Mambo mengine kutoka Zimbabwe

Juzi Waziri Mkuu wa Australia, John Howard, aliamua kusimamisha timu ya kriketi ya nchi hiyo kwenda kucheza nchini Zimbabwe. Howard anajua kwamba Mugabe anaupenda sana mchezo huu, kwa hivyo anadai kuwa timu ya Australia ikisafiri katika Zimbabwe, itasaidia siasa na urais wa Mugabe. Howard hataki kutetea maovu ya Mugabe.
Kwa kawaida mambo kuhusu michezo yanahitaji kuwa shughuli ya vyama vya michezo, lakini Howard alihisi kwamba alihitaji kuhusika (intervene). Je, unafikiri ni lazima uamuzi huu uwe ya chama cha kriketi cha Australia, ama unafikiri ni vizuri kuwa Waziri Mkuu aliingia kigambo hiki? Aidha, unafikiri kwamba jinsi nzuri ya kushinda Mugabe ni kuweka vikwazo (sanctions) kwa nchi hiyo ama kufanya hii itaongeza maumivu ya wananchi?

Sunday, May 6, 2007

Kusaidia Nchi ya Kenya

Kuna tofauti nyingi sana kati ya nchi ya Kenya na nchi za Kimagharibi. Kwa mfano barabara za Kenya zinaharibika na katika sehemu nyingi za Kenya hakuna barabara hasa barabara za lami. Pia katika sehemu nyingi za nchi hakuna umeme, gesi, petroli, hospitali, au maji safi. Je, unafikiri hivi ni vitu ambavyo ni lazima tuwasaidie watu wa Kenya au labda unafikiri kwamba tuache waendelea na desturi zao?

Kati ya nchi za Kimagharibi kuna mdahili kuhusu njia nzuri zaidi kusaidia nchi za Ulimwengu wa Tatu kama Kenya. Watu wachache walisema nchi za Kimagharibi ziipe Kenya pesa na ziambie kampuni za Kimagharibi kutega uchumi nchini Kenya. Lakini watu wengine wanasema kwamba njia nzuri zaidi ni kwa vyama vya kusaidia (kama Samaritan's Purse) na watu wenyewe waingie Kenya na kusaidia. Wanasema hivyo kwa sababu wanasema serikali ya Kenya ni fisadi na itapoteza pesa. Na watu wengine wanasema Kenya inaweza kujisaidia, ina pesa za kutosha na itasababisha taabu yenyewe. Wanasema pia ikiwa nchi za Kimagharibi watasaidia Kenya, watu wa Kenya watakuwa watumwa wa pesa za Kimagharibi na halafu hawatajaribu kujisaidia. Je unafikiri nini? Ni kweli kuna shida nchini Kenya ambazo ni lazima zirekebishe? Unafikiri njia ya kusaidia ipi ni nzuri zaidi? Kwa nini?

Sunday, April 29, 2007

Uchaguo Katika Marekani

Kwa sababu mimi ni mwanafunzi wa Uhisano wa Kimataifa, ningependa kuanza mazungumzo kuhusu siasi hapa Marekani. Baada ya kuandika kuhusu uchanguo unaokuja, nitaeleza maswali kuhusu Uchaguo wa Rais was Marekani Katika Miaka Mia Mbili na Nane. Ningependa kujua maoni ya wanafunzi katika darasa hili kuhusu watajaji kwa ofisi kwa wingi wa kushoto au "democrats."

Kwa wingi wa kushoto, watajaji wawili wakubwa ni Barack Obama na Hillary Clinton. Hillary ni mzungu tu lakini Barack (jina hili lina maana ya "blessed" katika Kiswahili) ni Mswahili nusu. Babake alizaliwa na aliisha katika Kenya na mamake alitoka jimbo la Kansas katika Marekani. Kila mtajaji alizaliwa katika Marekani kwa sababu ni uhitaji kukimbia kwa Rais wa Marekani.

Uchaguo hawa utakuwa muhimu sana kwa sababu kwa kawaida Rais wa Marekani ni mzungu na mwanaume, kwa sababu Hillary ni mwanamke na Barack ni Marekani Mwafrika. Ina maana ya ikiwa wingi wa kushoto inashinda uchaguo, kwa wakati wa kwanza katika historia ya Marekani, kutakuwa rais wa mwanamke au rais wa mweusi. Ni kitu kikubwa kabisa kwa sababu kisogoni cha Marekani kulikuwa kirahi sana dhidi ya watu wa mweusi kwanza na baadaye kirahi sana dhidi ya wanawake. Je, unafikiri mtajaji yupi atashinda uchaguo wa msingi wa wingi wa kushoto na kwa nini? Pia, nani atakuwa Rais wa Marekani katika miaka mia mbili na nane, mtu wa wingi wa kushoto au mtu wa wingi wa kulia? Unafikiri watu wa Marekani wanahitaji badilisho katika kiongozi wa serakali? Kwa nini?

Tuesday, April 24, 2007

Upimaji wa Dawa

Utaratibu kuunda dawa kutibu Ukimwi ni urefu na tatizo sana. Makampuni ya dawa kwa kawaida yanatoka Marekani au Ulaya wa Magharibi. Ili inawezekana makampuni ya dawa yauze dawa yao, kwanza inahitaji kupita majaribio mengi. Majaribio ya kwanza hufanyika na seli halafu na wanyama. Kama haya yanaendelea vizuri, dawa yanawezekana kujaribiwa katika binadamu. Ili upate matokeo mazuri katika muda mfupi, makampuni yanataka kufanya marajibio ya binadamu katika Waafrika kwa sababu watu wengi wana Ukimwi.

Pia, matokeo yanafanyika haraka zaidi inapotumiwa "placebo" kulinganisha na dawa mpya (badala ya dawa ambayo imeshatumiwa kutibu wagonjwa). Kawaida hii haingeruhusiwa katika Marekani ama Ulaya, lakini wanasayansi wanasema kwamba kwa sababu la Waafrika wengi hawawezi kupata tibu kwa kawaida, ni nzuri zaidi kwamba angalau nusu watapata dawa katika jaribio. Kuhusu nusu wengine, hawatakipoteza kitu chochote.

Wengine wanasema kwamba kutumia 'placebos' ni sawa kwa sababu itahimiza maendeleo ya dawa, halafu dawa mpya itapatikana mapema zaidi kwa matumizi ya wagonjwa. Je, mnafikiri ni ya maadili (ethical) zaidi kutumia placebos au kuwakimu dawa nyngine (the "basic minimum of care" inapatikana katika Marekani au sehemu za Afrika) watu wa kundi ya kulinganisha?

Friday, April 13, 2007

Mada ya Ardhi

Tafadhali msome kifungu kifuatacho:

Wawili wauawa Uganda
(Kutoka tovuti ya BBC 12/04/07)

Polisi nchini Uganda wameelezea kwamba watu wawili wameuawa katika mji mkuu wa nchi hiyo, Kampala, wakati wa maandamano ya kupinga mipango ya serikali ya kutaka kuugawa msitu mmoja nchini humo kwa familia moja yenye asili ya ki-Asia.
Polisi walifyatua risasi za kuwashambulia baadhi ya wa-Asia walioonekana.
Serikali ya nchi hiyo imekuwa ikipendekeza kuubadilisha msitu huo na kuwa kiwanda cha sukari, kwa kuugawa msitu huo kwa kampuni ya sukari nchini Uganda.
Kampuni hiyo imesema itatoa ajira nyingi na kusaidia kipato cha wananchi wa Uganda lakini wanamazingira wanasema mradi huo unaweza kusababisha kumomonyoka kwa ardhi.


Ardhi ya umma ianaleta vigambo vikubwa katika Afrika Mashariki kwa sababu baadhi ya watu hasa matajiri wanataka kuitumia ardhi kwa mashamba au kujenga majengo makubwa ya ofisi na nyumba. Je, unadhani ni muhimu zaidi kukinga mazingira au kufanya miradi ili nchi iweze kuharakisha maendeleo ya uchumi? Kwa nini unadhani wananchi wengi wa Uganda hawataki kiwanda cha sukari ambacho kingeleta ajira? Nani ana haki kuamua jinsi ardhi itumike, serikali au wananchi?

Friday, April 6, 2007

Chanzo cha UKIMWI

Kumekuwa na mjadala wa muda mrefu sana kuhusu chanzo cha ugonjwa wa Ukimwi (Aids). Wapo wanaosema kuwa ugonjwa huu ulitengenezwa na wanasayansi wa kimagharibi katika maabara ili kupunguza idadi ya watu katika nchi za ulimwengu wa tatu. Wengine wanasema kuwa ugonjwa huu umetokana na nyani. Aidha, kundi lingine linashikilia kuwa Ukimwi ni adhabu kutoka kwa Mungu kwa sababu watu wamekuwa wabaya na watenda dhambi. Wewe una maoni gani kuhusu jambo hili, na kwa nini?