Monday, May 14, 2007

Mambo mengine kutoka Zimbabwe

Juzi Waziri Mkuu wa Australia, John Howard, aliamua kusimamisha timu ya kriketi ya nchi hiyo kwenda kucheza nchini Zimbabwe. Howard anajua kwamba Mugabe anaupenda sana mchezo huu, kwa hivyo anadai kuwa timu ya Australia ikisafiri katika Zimbabwe, itasaidia siasa na urais wa Mugabe. Howard hataki kutetea maovu ya Mugabe.
Kwa kawaida mambo kuhusu michezo yanahitaji kuwa shughuli ya vyama vya michezo, lakini Howard alihisi kwamba alihitaji kuhusika (intervene). Je, unafikiri ni lazima uamuzi huu uwe ya chama cha kriketi cha Australia, ama unafikiri ni vizuri kuwa Waziri Mkuu aliingia kigambo hiki? Aidha, unafikiri kwamba jinsi nzuri ya kushinda Mugabe ni kuweka vikwazo (sanctions) kwa nchi hiyo ama kufanya hii itaongeza maumivu ya wananchi?

4 comments:

Jason said...

Kwa maoni yangu, ninahisi kwamba Howard alifuata njia sahihi alipozuia timu ya Australia kwenda nchini Zimbabwe. Nchi za ulimwengu zinahitaji kubidi nchi ya Zimbabwe kutoa dhalimu wao, ambaye ametawala nchi hiyo tangu ya mwaka wa 1980. Sasa, uchumi wa Zimbabwe umeharibika. Uvimbe umefika 2200%, na 80% ya wananchi hawana kazi. Wengi wanatoroka nga’ambo hasa Afrika Kusini. Wakati umefika ambao nchi za ulimwengu haziwezi kusimama kando zikiangalia maovu ambayo yanaendelea nchini Zimbabwe. Tunahitaji kutenda! Haki za binadamu zimefisidiwa na wengi wamefungwa zuizini bila jaribio. Ni muhimu kwamba michezo hasa kriketi isimamishwe kwa sababu ya mambo haya yanaendelea Zimbabwe. Tuwezi kuendelea kujistaresha wakati wananachi nchini humo wanapambana kuishi. Kwa hivyo nimefurahi kuwa Howard amechukua hatua hii. Chama cha Kriketi Duniani, kilikuwa kikitaka Australia kusafiri nchini Zimbabwe au kupasishwa adhabu ya kulipa fedha ya dola milioni mbili. Kwa hivyo ilikuwa ni afadhali Waziri Mkuu Howard ahusike.

Nadhani kwamba vikwazo si njia nzuri zaidi ya kujaribu kutoa Mugabe na kumaliza utawala wake. Vikazo vitauma uchumi na kuzidi matatizo ambayo yananendelea nchini humo. Pia vitauma wananchi zaidi kuliko serikali. Mugabe ameonyesha tayari kuwa hajali kuhusu wananchi wake, na yeye atakuwa na njia kupata bidhaa anayotaka. Kunahitaji kuwa maasi kutokana na wananchi wote wa Zimbabwe pamoja ili wawe na nafasi ya kutoa Mugabe. Nchi za dunia zinhitaji kuhimiza maasi na labda wanaweza kutuma majeshi yao kusaidia. Hasa Afrika Kusini inahitaji kuingia kati ya maneno hayo na Mbeki anapaswa kuacha kuhimiza Mugabe. Afrika Kusini inaumwa na wahamiaji haramu wengi kutoka Zimbabwe.

Kate said...
This comment has been removed by the author.
Kate said...
This comment has been removed by the author.
Kate said...

Ninakubaliana na vitendo vya Waziri Mkuu wa Australia. Ikiwa nchi kama Zimbabwe ina matatizo ya serikali, mara kwa mara vikwazo ni njia kupata matokeo. Ndiyo, na uamuzi huu, nchi ya Zimbabwe itaumiwa wakati inapoteza watalii na fedha, lakini ikiwa dunia linaigiza kama hakuna mgororo mkubwa sana, vitu vitakaa mbaya sana huko. Kwa hivyo, uamuzi huu kuzuia kriketi cha Australia kwenda Zimbabwe ni ngumu kufanya lakini ni haki.

Ikiwa maumivu ya wananchi yanapata mbaya zaidi, angalau maumivu yatalazimisha kupata bora. Wakati wewe ni mwanasiasa, unahitaji kutengeneza uamuzi ngumu, na ni muhimu sana kukumbuka kwamba wakati wengine, uamuzi wa haki ni ngumu sana kufanya.