Friday, April 13, 2007

Mada ya Ardhi

Tafadhali msome kifungu kifuatacho:

Wawili wauawa Uganda
(Kutoka tovuti ya BBC 12/04/07)

Polisi nchini Uganda wameelezea kwamba watu wawili wameuawa katika mji mkuu wa nchi hiyo, Kampala, wakati wa maandamano ya kupinga mipango ya serikali ya kutaka kuugawa msitu mmoja nchini humo kwa familia moja yenye asili ya ki-Asia.
Polisi walifyatua risasi za kuwashambulia baadhi ya wa-Asia walioonekana.
Serikali ya nchi hiyo imekuwa ikipendekeza kuubadilisha msitu huo na kuwa kiwanda cha sukari, kwa kuugawa msitu huo kwa kampuni ya sukari nchini Uganda.
Kampuni hiyo imesema itatoa ajira nyingi na kusaidia kipato cha wananchi wa Uganda lakini wanamazingira wanasema mradi huo unaweza kusababisha kumomonyoka kwa ardhi.


Ardhi ya umma ianaleta vigambo vikubwa katika Afrika Mashariki kwa sababu baadhi ya watu hasa matajiri wanataka kuitumia ardhi kwa mashamba au kujenga majengo makubwa ya ofisi na nyumba. Je, unadhani ni muhimu zaidi kukinga mazingira au kufanya miradi ili nchi iweze kuharakisha maendeleo ya uchumi? Kwa nini unadhani wananchi wengi wa Uganda hawataki kiwanda cha sukari ambacho kingeleta ajira? Nani ana haki kuamua jinsi ardhi itumike, serikali au wananchi?

4 comments:

Daudi said...

Ninafikiri ni muhimu sana kukatiana kati ya mazingira na shughuli. Kwa hakika, inanonekana kwamba heri kuwa na kiwanda cha sukari kuliko msitu kwa sababu watu wengi wangepata ajira. Lakini, watu wanahitaji kugundua kwamba matatizo mengi yanaibuka baada ya kubomoa misitu. Nyumba za wanyama nyingi zitaharibika na mazingira yote yanaathirika.

Aidha, watu wengi ambao wanaishi karibu na msitu wanategemea msitu kupata kuni, chakula na kadhalika. Kwa hivyo ikiwa watu hawa hawapati kazi kutoka kiwanda cha sukari, hawatakuwa na jinsi nyingine ya kuishi.

Kwa hivyo, ni ngumu kusema nani ana haki kuamua jinsi ardhi itumike kwa sababu ni kweli ardhi ni raslimali ya serikali lakini jinsi ardhi inatumika inaathirika wananchi wengi. Kwa hivyo lazima serikali iongee na wananchi kabla ya kufanya uamuzi huu.

Claire said...

Kitu muhimu sana ambacho watu wachache wanaelewa ni kwamba ni lazima ukinge mazingira ili uzidi maendeleo ya uchumi. Bila ardhi yenye hali nzuri, hakuna jinsi ya kizao.

Serikali ya Uganda ni jamhuri, halafu inaigiza katika mambo ya wananchi wao. 82% ya Wauganda wanafanya kazi ya kilimo. Kwa hivyo ni muhimu sana serikali inaunda kazi nyingi katika eneo hili. Lakini pia ni muhimu serikali inahakikisha ikuwe mashamba mengi na mbalimbali yenye mabuana tofauti. Buana mmoja wa kigeni ambaye analima "cash crop" tu sio mzuri kwa uchumi au kwa mazingira.

Kate said...

Nakubali na Daudi kwamba ni muhimu sana kukatiana baina ya watu wa mazingira na watu wa shughuli, lakini nakubali pia na Claire kwamba bila mazingira mzima, hakuna nafasi au mahali kwa kiwanda cha sukari kujengwa.

Kwa hiyvo, ningesema ni muhimu zaidi kuafua mazingira ni kunge ya maisha wote. Pengine watu na fedha nyingi wanaweza kufanya kiwanda cha sukari mbali ya msitu huu. Yaani, nafikiri kuna njia kutengeneza watu wote wanafurahi na kuendelea maendeleo ya uchumi.

Ninaamania wananchi wa Uganda wana haki kuamua ikiwa majengo yatajengwa. Nafikiri pia watu wengi hawataki kiwanda hiki huko kwa sababu wanajua bila mazingira na afya, shughuli itakufa na watu watapotea kazi zake na halafu, dunia ingekuwa na mazingira mabaya sana na watu wote bila njia kufanya pesa kusabibisha familia yao.

Joe said...

Ninaamini kwamba mazingira ni muhimu sana, lakini pia uchumi ni muhimu pia. Hasa katika nchi za Afrika Mashariki, kwa mfano Uganda, uchumi ni mbaya sana, na maisha ni magumu kwa watu wengi. Ingawa kiwanda cha sukari kitaharibia msitu, kitaauni kazi nyingi. Hiki ni kitu kizuri. Lakini kuna vinyume vibaya kutoka kujenga kiwanda, kama nyumba za wanyama nyingi zitaharibika (kama Daudi alisema). Pia kuharibia msitu kutasababisha umomonyoko ambao utaharibia mashamba yanayoduru msitu.

Kwa sababu kuna fanaka na hasara pia kutoka kuugawa msitu, mimi siwezi kuamua kufanya nini. Lakini kuhusu nani aamue, serikali ama wananchi, ninafikiri kwamba wananchi waamue. Kama Claire alisema, Uganda ni jamhuri, kwa hivyo watu wanaweza kuamua kitu ambacho wanataka kufanya. Pia, kwa sababu watu ambao wanalalimika juu ya kuugawa msitu ni maskini. Kwani kiwanda kitawasaidia, kama hawakitaki waamue kwamba hakitajengwa.