Tuesday, October 30, 2007

Kumkaribisha Emily na kujitambulisha

Karibu sana Emily katika mawasiliano yetu haya. Ni furaha yetu kuwa nawe katika blogu ya Kiswahili. Aidha, asante kwa kujitambulisha kwetu. Naamini kwamba washiriki wengine nao watajitambulisha ili ujue unawasiliana na nani (mimi naamini wote mwanijua).

Hongera kwa uchaguzi wenye amani na utulivu. Je, waweza kusema machache kuhusu serekali ya wanafunzi hapo chuoni? Kwa mfano, inajumuisha viongozi wangapi na majukumu yao ya kimsingi ni nini? Wanayatekeleza vizuri? Siasa za ukabila zinajitokeza ndani yake au la? Hatimaye kwa nini wewe hukugombea nafasi yoyote? Baadaye, tutatarajia wanafuzni wa hapa Stanford kutueleza kama kuna mfumo kama huo huku.

Usiku mwema.

5 comments:

Jason said...

Pia mimi ningetaka kukusalimia Emily na kukukaribisha katika mawasiliano yetu tuliyoanza mwaka uliopita tulipokuwa katika darasa la pili la Kiswahili. Kwanza kabla ya kuendelea na mazungumzo yetu, ningetaka kujijulisha kwako. Mimi ni Jason Dunford, mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa biolojia wa binadamu na Kiswahili hapa chuoni na pia mwakilishi wa timu ya Stanford ya uogeleaji. Kwa hakika, mimi ni raia wa Kenya, mojawapo wa wananchi wazungu wachache wa nchi yetu, na ninaishi mjini Nairobi na wazazi wangu ambao wanafanya kazi katika kampuni ya hoteli iliyoanzishwa na Babangu na rafiki yake miaka thelathini iliyopita. Hoteli maarufu zaidi ya kampuni hii inaitwa ‘Carnivore’ na iko katika eneo la Langata.

Juu ya kuwakilisha timu ya Stanford katika uogeleaji, mimi ni mwakilishi wa timu ya Kenya na nitakuwa nikishindana katika Michezo ya Olimpiki mwaka ujao. Natarajia nitaweza kushinda medali moja na kuleta utukufu mwingi nchini kwetu.

Nilipofika Stanford niliamua kusoma Kiswahili kwa sababu uwezo wangu kutumia lugha hii ilikuwa mbovu na nilikuwa na soni kusema kwamba mimi ni raia wa Kenya. Sasa kwa upole nimeanza kurekebisha hali hiyo na ninaboresha matumizi yangu ya lugha. Kwa hakika, niliporudi Kenya baada ya Michezo ya Kiafrika ya mwezi wa saba wa mwaka huu, nilifurahi kuweza kuhojiwa katika Kiswahili kwa mara yangu ya kwanza!

Hatimaye kuhusu swala la mfumo wa uchaguzi wa viongozi wa wanafunzi hapa Stanford. Najua kwamba kuna uchguzi kila mwaka lakini si kitu kikubwa na hata leo sijui mwanafunzi yupi ni kiongozi wetu.

Lakini kufanana na uchaguzi wa wanafunzi, katika timu yetu ya uogeleaji, kila mwaka tuna uchaguzi wa viongozi wetu. Mwaka huu tuna watatu, moja Mmarekani, moja Mkanada na moja Mbrazil na wanaendelea kufanya kazi nzuri sana. Kazi zao zinashirkisha kuwasiliana baina ya waogeleaji na makocha wetu, kupanga na kuongoza mikutano ya timu na kuhimiza timu katika mazoezi na mashindano. Naamini kwamba uongozi wa viongozi hawa watatu utatusaidia sana tukijaribu kushinda ushindi wa kitaifa wa vyuo vikuu.

Daudi said...

Hata mimi, ningetaka kukukaribisha Emily na wanafunzi wengine wa chuo kikuu cha Egerton na kujijulisha kwenu.

Mimi ni kaka mdogo wa Jason kwa hivyo malezi yetu ni sawa. Nilizaliwa mjini Nairobi na kusoma katika shule ya msingi huko kabla ya kuanza masomo yangu ya sekondari katika Uingereza. Sasa, mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa pili hapa chuoni kwa Stanford.

Mimi pia ni mwogeleaji na ninawakilisha timu ya Stanford na juu ya hiyo timu yetu ya taifa. Nilianza kuogelea nilipokuwa mdogo sana na kuendelea na mchezo huu mpaka sasa. Daima, nimeota kuwakilisha Kenya katika mchezo wa Olympiki na japo sijafuzu tayari natarajia kwamba nitapata nafasi ya kushindana mwaka ujao.

Kwa mada tofauti, nimefurahi sana ya kuwa na nafasi ya kuongea na wanafunzi wa kenya katika mtandao na ninatarajia kwamba tunaweza kuwa na mazungumzo ya kufurahisha baadaye.

mohochi said...

Binafsi nafurahishwa mno na yale ninayoyasoma humu. Emilly wajulishe wenzako huko kwamba tuna hamu kuu ya kuyasikia waliyonayo. Sasa unawajua washirika wa blogu hii ya kiswaz na waweza kuandika bila wasiwasi upatapo nafasi. Aidha, kuna blogu ya wanafunzi wa mwaka wa pili (wanafunziwakali.blogspot.com) na wanafunzi wa Egerton mnaalikwa kujiunga nao pia.

Jason said...

Imefika Jumapili jioni tena na ninaketi chumbani mwangu nikijaribu kuandika kitu kizuri ambacho labda kitawasisimua kidogo. Jumatano ya wiki iliyopita tulikuwa na mashidano ya uogeleaji dhidi ya chuo kikuu kingine kinachoitwa “Cal”, na tuliwachapa waogeleaji wao vibaya. Binafsi, mimi nilishinda mbio tatu ambazo zilinifurahisha sana hasa kwa sababu nilikuwa na kikohozi kibaya na pia nyakati nilizoogelea zilikuwa haraka na sikutarajia kuogelea kwa upesi huo kwa kuwa bado tunaendelea na mazoezi magumu, ambayo ni kawaida katika mwanzo wa majira ya uogeleaji yetu. Kwa hivyo makocha wangu walifurahi sana na matendo yangu na ninatamani kwamba nitaendelea kuogelea vizuri katika majira yote na nitakapopumzika zaidi kabla ya mashindano yangu makubwa mwaka ujao, nyakati zangu zitakuwa bora zaidi.

Wikendi hii nilikuwa na mambo mengi ya kujishughulisha na kazi nyingi ya kufanya. Timu yetu tena ilikuwa na kurutu wanne wa uogeleaji, ambao mimi nimefurahi kusema kwamba wote watakuja hapa mwaka ujao, kwa hivyo tulipaswa kuwaonyesha chuo kikuu chetu na kulikuwa na shughuli mbalimbali ya timu. Kwa sababu wote wamesema wataandikia hapa mwaka ujao, inaonekana kwamba bila shaka tuliwaonyesha wakati mzuri.

Sawa, hivyo ni vitu vichahce ambavyo vilitukia wiki iliyopita. Wiki ijayo timu yetu inashindana mjini Los Angeles katika shindano linaloshirkisha takriban vyuo vikuu ishirini, linaloendelea kwa siku tatu na ninataraji kwamba timu itaogelea vizuri.

Hatimaye, kuhusu swala lingine nililosomea katika mtandao, kwamba vita vibaya vinaendelea mjini Mogadishu nchini Somalia na nigetaka kuwauliza maswali machache kupata maoni yenu. Je, mnafikiri siku moja Somalia itaweza kuwa na amani na kuacha vita? Kuna njia ya kupata amani nchini humo au la? Viongozi duniani wanaweza kufanya nini kusaidia Somalia kupata amani?

Daudi said...

Inaonekana kwamba kila wakati ninafuata Jason katika blogu hii na kwa sababu tunaishi pamoja na tuko pamoja katika timu sawa ya uogeleaji, kwa kawaida habari zake ni habari zangu pia. Kwa hivyo leo sitaki kutaja vitu alivyoandika lakini kuandika kuhusu maswala tofauti.

Sasa hivi nimerudi kutoka utendaji wa ngoma ambapo wanafunzi wa chuo kikuu hiki walikuwa wakicheza ngoma za tanzu mbalimbali. Wachezaji wa ngoma wa chama kimoja walicheza ngoma wakiwa katika sakafu, tanzu hii inaitwa “breakdancing” katika kiingereza na ilinifurahisha sana. Wengine walikuwa wakifanya ngoma katika mikono na walipendwa zaidi na hadhira. Kwa hakika, mtu akiingia bwalo hilo wakati wa utendaji, angefikiri kwamba karamu ikiwa ikiendelea kwa sababu watazamaji walikuwa wakipiga kelele jingi na kujirusha kwa miguu.

Ingawa ni swala mbalimbali kabisa, kuhusu maswali ya Jason, nafikiri kwamba wakati utakuja ambao watu wa Somali watagundua kuwa maendeleo ya nchi si ya kupigana kila siku lakini ni kuafikiana na wananchi wengine na kuunga mikono ili wachukue hatua za kwenda mbele.