Tuesday, November 13, 2007

Wikendi yenu na maswala ya Somalia

Habari za leo?

Kwanza kabisa napenda kusema tena kwamba nafurahishwa na maendeleo yenu katika matumizi ya lugha. Aidha, nimeweza kujua mengi mliyoyafanya wikendi iliyopita. Je, Daudi wewe hupenda kucheza ngoma pia? Jason, kwa kawaida kila mwaka wanafunzi wangapi wapya hujiunga na timu yenu kali ya uogeleaji? Hongera sana kwa kuboresha wakati wako katika uogeleaji.

Kuhusu, Somalia mimi naamini kwamba hakuna marefu yasiyokuwa na mwisho. Kwa sababu hiyo, ipo siku Somalia itajua maana ya amani. Hata hivyo, nadhani kuwa jamii ya kimataifa yapaswa kuwasikiliza watu was nchi hiyo, na nyingine nyingi zilizo vitani, kabla ya kuyafkikia maamuzi katika hoteli mbalimbali mikutanoni. Kwa kufanya hivyo na kwa kushirikiana nadhani kuwa ufumbuzi wa matatizo yanayoikabili utawezekana.

Nawatakia safari njema ha[po kesho na mpatapo nafasi andikeni kuhusu mashindano yenu-hata kama ni kwa muhtasari tu.

No comments: