19/06/07
Leo ni leo. Niliamka kwenda kuogelea mapema na nilifanya vizuri sana licha ya mwili wangu ambao umekamatwa na mafua. Baada ya mazoezi, nilirudi chumba changu kulala kidogo lakini usingizi wangu ulikuwa mkubwa kwa hivyo nilikaa kitandani kwa masaa manne! Hatimaye nilipoamka, niliandaa chakula cha mchana na nilikikula na rafiki yangu. Sasa ninaketi kwa kompyuta nikifanya mazoezi ya hii lugha safi na ninasikitika darasa letu la mwaka uliopita. Tafadhali muandike vitu vichache kueleza safari zenu!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
8 comments:
Asante sana jason. Nakutakia wewe na mdogo wako mazoezi mema. Mimi sijaanza likizo kwa kweli. Ni jana tu nilipomaliza kuweka alama zenu na za wanafunzi wengine katika axess. Sasa nataka kuanza kazi ya kuandaa hojaji (questionnaire) ya utafiti mdogo nitakaoufanya Afrika Mashariki. Aidha, napaswa kuirekebisha makala moja niliyoandika ili ichapishwe katika kitabu. Je, tutapata fursa ya kunywa kahawa nanyi kabla sijaondoka kwenda Kenya? Wengine mlisafiri salama? Sijasahau msamiati wa wiki ya mwisho pamoja na matusi-nitayaweka yote katika coursework na kuwafahamisha hivi karibuni.
Baadaye basi.
Inaonekana hakuna mtu anataka kutueleza kuhusu likizo yake ya kiangazi? Juzi nilijaribu kutundika insha za wengine katika wavuti wetu swahililanguage.stanford.edu lakini kuna matatizo ya kiufundi. Nitajaribu tena kabla ya mwisho wa wiki hii.
Kila la heri.
Hamjambo rafiki zangu za darasa letu la Kiswahili. Natarajia kwamba kila mtu anaburudika au kujifurahisha tu. Bado niko hapa chuoni kwa Stanford pamoja na kakangu na tunaendelea na mazoezi yetu.
Tangu muhula uliopita ulipoisha, sijafanya vitu vya kufurahisha vingi ila wikendi iliyopita mimi na Jason tulisafiri jijini San Francisco kukutana na kifunguamimba wa familia yetu. Sasa siku tisa tu zinabaki mpaka nitatoroka kwenda Algeria. Kwa hivyo, wiki ijayo, ningependa sana kukutana na wewe mwalimu kunywa chai au kahawa na kubalishana habari za likizo hii. Tuzungumze na barua pepe.
Habari zenu wenzangu. Poleni kuchelewa kuandika tangu siku ile. Likizo yangu inaenedelea vizuri hasa uogeleaji. Niliogelea katika mashindano wikendi iliyopita na kufurahi na muda zangu. Wikendi ijayo nina mashindano mengine katika Santa Clara na waogeleaji wengi wazuri watakuwa wakishindana. Ninataraji kwamba nitawachapa wote.
Sawa, tutazungumza baadaye. Kila la heri
Leo nimejaribu kuelewa shairi la Mwalimu Mohochi inaloitwa 'Wawindaji'. Kuna msamiati mwingi ambao sielewi, lakini ninadhani kwamba wawindaji wanaheshimiwa katika jamii kwa sababu ya uhodari wao na pia kwa sababu wanalisha wenzao katika jamii. Lakini nyumbani halisi kwa wawindaji ni porini.
Kama mmesoma shairi hili, tafadhali muandike kitu. Halafu, mwalimu kama una nafasi, ungeweza kueleza maana lake la kweli.
Habari za leo? Nafurahi kuona kuwa tunaendelea kuwasiliana kupitia njia hii. Nitatoa maoni kuhusu shairi langu baada ya wengine kusema wanachofikiri. Jason, mnaogelea Santa Clara siku gani? Mimi naondoka Jumatatu jioni kwenda Kenya. Nadhani tunaweza kukutana na kunywa kahawa, pamoja na kubadilishana habari kama alivyopendekeza Daudi. Je, ni siku gani ya wikendi mtakuwa na nafasi?
Nakubali pongezi pamoja tukuze kiswahili
Post a Comment