Wikendi hii, nimeshughulika sana kwa sababu nimehitaji kufanya kazi zangu za chuo na vile vile timu yetu ya uogeleaji imekuwa na kurutu katika wikendi yote. Aidha, tulikuwa na mazoezi ya uogelaji jumamosi asubuhi na yalifuatwa na finali ya kombe cha dunia cha ragbi ambacho Afrika Kusini ilishinda.
Kwahivyo, jumamosi baada ya mazoezi, chamshakinywa na mchezo wa ragbi, nilienda kucheza 'frisbee' pamoja na timu na kurutu. 'Frisbee' ni mchezo ambao watu wanatupana diski inayoweza kuruka mbali sana. Baada ya mchezo huu, sisi wote tulienda nje kula katika mkahawa wa Meksiko. Baada ya chajio, tena pamoja tukaenda kucheza mchezo mwingine amabo katika kiingereza unaitwa 'bowling.' Katika mchezo huu, unahitaji kutupa mpira mgumu ili uangushe mingi ya miti kumi unayoweza.
Lakini, usiku wa jumamosi, baada ya kucheza 'bowling,' nilianza kuhisi vibaya, kwa hivyo niliamua kulala mapema wengine walipokuwa wakisherekea.
Sasa, asubuhi ya jumapili, ninahisi bora kuliko jana usiku lakini nina kazi nyingi ya kuandika kabla ya mwisho wa wikendi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
7 comments:
Wikendi yangu ilianza mapema Jumamosi kwa sababu nilihitaji kuamka saa moja kasa robo ili nienede kufanya mazoezi ya uogeleaji na timu yangu ya Stanford. Baada ya kufika bwawa na kujitayarisha, sisi huingia maji saa moja na nusu. Jumamosi hii tulikuwa na mazoezi magumu ya miguu, ambayo yalinichokesha sana.
Baada ya mazoezi waliowengi wa timu yetu hula chamshakinywa pamoja katika mkahawa mmoja wa chuo. Hasa kwa sababu tulikuwa na kurutu watatu wa uogeleaji wikendi hii, timu yote ilikuja kula. Chakula ni hicho cha kawaida cha chamshakinywa hapa Marekani,na kinashirikisha bekoni, mayai, maji ya matunda, uji na kadhalika.
Tulipomaliza kula, kakangu nami tulienda kuangalia katika runinga finali ya kombe ya dunia ya raga baina ya Uingereza na Afrika Kusini. Kwa sababu sisi hushangilia Afrika Kusini katika raga ya dunia, tukafurahi sana timu hii iliposhinda na kuleta kombe hii kwenye Afrika.
Mechi hii ilimaliza saa mbili kasa robo, na tukaunga timu na kurutu tena, ambapo wlikuwa wakicheza mchezo wa “frisbee”. Tulijistarehesha na michezo huu mpaka saa kumi jioni, tuliporudi buenini kupumzika kidogo kabla ya kwenda nje kula chakula cha jioni.
Tukala chakula cha jioni katika hoteli inayoitwa "Celia’s" ambayo inahuduma chakula Kimeksiko. Mimi, kama kitoweo, nilikula kuku, nyama ya ng’ombe na maragwe, na kama chakula kikuu, wali na chapati. Kweli nilikinai!
Watu waliposhiba, tulienda kujistarehesha na mchezo wa “bowling” mjini Palo Alto na hatimaye tukarudi chuoni kulala.
Kurutu waliondoka mapema asubuhi ya Jumapili na ninaadhani kwamba walipenda chuo chetu na ninatarajia kwamba wataamua kuja hapa mwaka ujao.
Jumapili ilipofika, nilichelewa kidogo kuamka kwa sababu ya uchovu unaosababsihwa na shughuli za Jumamosi. Jumapili imekuwa siku ya kazi na kweli kazi hii ni karibu kunilemea. Lakini ni lazima niendelee kupambana na kujaribu kuimaliza.
Naam,
nami pia nitaandika kuhusu wikendi yangu baadaye.
Habari za saa hizi? Niliahidi kuandika kuhusu wikendi yangu (iliyopita). Wikendi iliyopita ilikuwa njema kabisa. Kama mjuavyo, nilisafiri hadi jijini New York kujiunga na wanachama wengine wa chama cha Masomo ya Afrika, "African Studies Association" katika kongamano lao la mwaka huu. Kwa hakika, mkutano ulihudhuriwa na watu wengi sana kutoka pembe zote za nchi ya Marekani pamoja na sehemu nyingine za dunia. Nilifurahi sana kukutana na kuzungumza na watu kadhaa ninaowajua ambao nilikuwa sijawaona kwa muda mrefu sana. Baadhi yao ni walimu wa Kiswahili kwa hivyo, mbali na maswala ya kijumla kuhusu masomo ya Kiafrika, tuliweza kujadili pia mammbo yanayohusiana na Kiswahili.
Baada ya kurejea hapa chuoni niligundua kuwa kazi ilikuwa imerundikana si haba. Kwa sababu hiyo wiki hii yote imekuwa wiki ya heka heka nyingi sana. Hata sasa bado kuna mengi ambayo sijayamaliza. Naamini kuwa nitayatekeleza ninayopanga kuyatekeleza.
Ni wazi kuwa wikendi iliyopita ilikuwa ya shughuli nyingi kwetu sote. Je, hii mnatarajia iwe vivyo hivyo?
Baada ya kuzungumza kuhusu wikendi hii, ningependa mtoe maoni yenu kuhusu hali ya siasa nchini Kenya. Mnadhani kuwa nani atashinda uchaguzi ujao na kwa nini?
Binafsi, nadhani kwamba kila wikendi iwe vivyo hivyo hapa chuoni na ni maisha ya kawaida katika chuo kikuu kizuri kama hiki. Hasa kwa sababu sisi wote hatutaki kuwa wavivu, na tunapenda sana kukidhi wengine, tunapanga vitu vingi vya kufanya hata kama wakati ni haba. Methali moja, “Mtaka cha mvunguni sharti ainame,” na inatunaonya kwamba uvivu hauna manufaa na hakuna faida bila sadaka. Inatunasihi kufanya bidii tukitaka kufaulu maishani na kutekeleza vitu vya maana. Hata saa hii, nikiandika maneno haya, tayari nimefanya vitu vingi katika Jumamosi hii. Nimefanya masaa mawili ya uogeleaji, tumekuwa na mkutano wa timu, na nimefanya masaa kadhaa ya kazi ya shule. Bado haijafika saa kumi!
Sasa kuhusu mada tofauti kabisa: siasa nchini Kenya. Wiki iliyopita nimekuwa nikisoma magazeti ya Nation na Standard katika Mtandao, na nimeshangaa kusoma kwamba wengi nchini Kenya wanadhani kwamba Raila atashinda uchaguzi wa mwaka huu na kuwa rais wa nne wa nchi yetu. Taarifa ambayo ilitolewa na kampuni ya Steadman kuhusu maoni ya wananchi kuhusu uchaguzi, imeonyesha Raila akiongoza mbio wa rais na pointi hamsini dhidi ya thelathini na tisa ya Kibaki.
Lakini, jana Raila alikuwa akitembelea wilaya ya kati na alikutanwa na uhasama mwingi kutokana na wakazi wa wilaya hiyo. Gazeti la Nation imerepoti kwamba watu walikuwa wakipiga kelele kubwa wakisema, ““Yote yawezekana bila Raila, yote yawezekana bila Ruto.” Ni kweli kwamba wilaya hii ni ya Kibaki, kwa hivyo ODM hawangetarajiwa kupata watu wengi ambao wanamshagilia, lakini inaonyesha kwamba uchaguzi huu utakuwa kusisimua. Kwa sasa, sidhani kwamba watu wanajua kwa kweli nani ataushinda.
Inaonekana kwamba kama kawaida watu wengi watampigia mtu maalum kura kwa sababu ya kabila na si kwa sababu ya sifa za mtu huyu. Nikisoma magazeti, ninaamini kwamba Raila anafanya zaidi kuliko Kibaki kushawishi watu kumpigia kura kwa sababu ya sera zake. Amekuwa akishutumu serikali ya Kibaki kwa sababu ya kuwa fisadi na kula pesa nyingi za umma. Labda atafaulu, na Wakikuyu wachache watampigia kura na atasababishwa kushinda. Binafsi, sina pendekezo la Kibaki au Raila, natarajia tu huyu ambaye atashinda atakuwa rais mnyenyekevu, mwaminifu na mnyofu.
Jason,
Nimeyapata maoni yako vizuri sana. Kwa kweli inasikitisha kuona kuwa watu wengi hawajali sifa za mgombea wa kiti muhimu kama cha urais, bali wanajali zaidi kabila lake. Ni matumaini yangu kuwa vijana wa siku hizi wataibuka kuwa makini zaidi kwa hilo na kutuondoa ukabilani.
Kuhusu kazi za chuoni, ni vizuri pia kusikia kwamba mnafurahia kazi za chuo, japo nyingi. Nimewaalika wanafunzi wa chuo kikuu cha Egerton kujiunga nasi na nadhani tutaanza kusikia maoni yao hivi karibuni. Wakishajisajili katika blogu yetu na sisi wote kujitambulisha, tutaanza kuzijadili mada maalu.
Baadaye,
Ninaafikiana na Jason kuhusu wikendi za chuo kikuu chetu. Kila wikendi nina shughuli nyingi za kumaliza kabla ya kuanza wiki nyingine. Kwanza, katika wiki najaribu kulala mapema kwa sababu ya kuamka mapema kwa hivyo pamoja na madarasa na uogeleaji sina muda ya kutosha ili nimalize kazi zangu za nyumbani. Mradi, kazi zangu zinazidi mpaka wikendi na jumamosi na jumapili nahitaji kujikaza sana. Zaidi, kwa kawaida si kazi za shule ninahitaji kufanya katika wikendi. Kama Jason, kila jumamosi asabuhi nina mazoezi za uogeleaji na kufuata na utenzi wa timu yetu. Kwa mfano wikendi iliyopita tulikuwa na utenzi mwingi kwa sababu ya kurutu na jana tulikuwa na mkutano wa timu yote. Hatimaye, katika wikendi napenda kufanya kitu na mpenzi wangu kwa sababu huwa simoni sana katika wiki. Kwa hivyo, hata wikendi sina muda nyingi ya kupumsika lakini ni hali ya maisha na ninfikiri kwamba methali Jason aliyotumia ni mwafaka.
Kuhusu mada nyingine ya uchaguzi wetu wa rais, pia mimi nadhani kwamba ni mbio baina rais wa sasa Mwai Kibaki na yule mwanasiasa mwingine Raila Odinga. Juzijuzi nimekuwa sijafuata habari nyingi kutoka Kenya lakini najua sasa hivi inaonekana kwamba Raila ana faida juu ya Kibaki. Aidha, tena kama kawaidi inaonekana kwamba watu watachagua rais kwa sababu ya kabila yake kwa hivyo waliowengi wa Kikuyu watapiga kura kwa Kibaki na waliowengi wa Luo watapiga kura kwa Raila. Sasa, wagombea wanahitaji kuwashawishi wao ambao si wakikuya au waluo, na ninafikiri kwamba Raila anafanya bidii kupita Kibaki.
Kwa hivyo, siwezi kusema nani atashinda kati ya Kibaki na raila ama nani atakuwa rais mzuri kuliko mwingine. Lakini ninyakini kwamba rais wetu wa miaka mitano ijayo atakuwa Kibaki tena au Raila.
Hamjambo wapenzi wa Kiswahili popote mlipo sasa.Nimejiunga hii leo na blogu ya Wanafunzi wa Kiswahili na nafurahia mawasiliano yaliyopo kwa jumla.Mimi ni mwanafunzi wa fasihi ya Kiingereza na lugha ya Kiswahili katika Chuo Kikuu Cha Egerton(KENYA)
Wikendi yangu ilianza mapema usiku wa Ijumaa katika zile harakati za kuzihesabu kura za wanafunzi kwani nilikuwa nimeteuliwa kama katibu katika uchaguzi wa chama wakilishi cha wanafunzi(SUEU).Uchaguzi huo ulikuwa umefanyika mchana wa Ijumaa.Baada ya kuwatangaza washindi usiku wa manane,sherehe na burudani za washindi zilianza papo hapo ingawa nilikuwa mchovu kiwango cha kutoweza kujiunga na wenzangu.
Mchana wa jumamosi ulikuwa wenye tafrija nyingi ambazo nilihusika kwa kiwango kikubwa ingawa si kwa ndani sana.Usiku huo nilikuwa kwenye tamasha la "Trinity Dancers" ambapo jukumu langu kuu lilikuwa kuwatumbuiza wageni kwa kusakata ngoma na midundo ya Kiafrika kweli.(mimi hucheza ngoma za kitamaduni na mziki wa kizazi kipya vilivyo).Tamasha hiyo iliisha asubuhi.
Jumapili nilienda kanisani katika ibada ya pili,kisha nikahunduria kipindi cha ubatizo chuoni.Baada ya chakula cha mchana,mimi pamoja na makatibu wenzangu tuliohusika katika kura za uchaguzi wa wanafunzi wawakilishi tulienda kupanda miti katika "botanical garden" iliyopo chuoni kwa kuiendesha shughuli hiyo ya uchaguzi kwa amani bila vurugu kutoka kwa wanafunzi.Usiku huo nilisomea mjarabu niliokua nao leo mchana.
Post a Comment