Friday, April 6, 2007
Chanzo cha UKIMWI
Kumekuwa na mjadala wa muda mrefu sana kuhusu chanzo cha ugonjwa wa Ukimwi (Aids). Wapo wanaosema kuwa ugonjwa huu ulitengenezwa na wanasayansi wa kimagharibi katika maabara ili kupunguza idadi ya watu katika nchi za ulimwengu wa tatu. Wengine wanasema kuwa ugonjwa huu umetokana na nyani. Aidha, kundi lingine linashikilia kuwa Ukimwi ni adhabu kutoka kwa Mungu kwa sababu watu wamekuwa wabaya na watenda dhambi. Wewe una maoni gani kuhusu jambo hili, na kwa nini?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
11 comments:
Ugonjwa wa Ukimwi umetokana na nyani kwa sababu watu wa misitu katika Afrika ya Kati hula nyama ya nyani. Wanasayansi wametambua virusi katika nyani ambavyo vinafanana na virusi vya ukimwi katika binadamu. Kwa hivyo, kuna yamkini kubwa kuwa virusi hivi katika nyani viliruka kipingo cha spishi na baada ya kubadilika, vilipata uwezo kusababisha ugonjwa katika binadamu.
Watu ambao wanasema kuwa ugonjwa huu ulitengenezwa na wanasayansi wa kimagharibi ni wajinga kwa sababu kuna watu katika nchi za kimagharibhi ambao wameuawa na ugonjwa huu. Sidhani kwamba wanasayansi wangetaka kuua wananchi wenzao. Pia, wakati mwingine virusi vya Ukimwi vinadumu mpaka miaka ishirini kusababisha ugonjwa wa Ukimiwi ambao unaua mtu. Kwa hivyo, iwapo nchi za kimagharibi zingetaka kupunguza idadi ya watu katika nchi za ulimwengu wa tatu, zingetumia njia rahisi kama mabomu ya kinuklia.
Hatimaye siwezi kukubali kuwa ugonjwa huu ni adhabu kutoka Mungu. Nieleze kwa nini katika karne iliyopita, ghafla Mungu aliamua kuadhibu binadamu? Tumekuwa tukipigana kwa karne nyingi na pia nilidhani Mungu anasamehe. Aidha, kuna magonjwa mengine mengi katika ulimwengu wetu ambayo watu hawasemi ni adhabu kutoka Mungu.
Sasa ni ngumu kuandika jibu asilia baada ya kusoma kifungu ambacho kimeandikwa na Jason, kwa sababu maoni yetu ni sawa.
Aidha ninafikiri Ugonjwa wa Ukimwi umetokana na nyani katika Afrika ya Kati. Sijui mingi kuhusu ugonjwa huu lakini ninajua wamba kuna buruhahi sadikifu kudikeza kuwa Ukimwi uliibuka kwa jinsi hii.
Hawa watu ambao wanadai kwamba ugonjwa huu ulitengenezwa na nchi za kimagharibi hawana buruhahi ata kuauni dai lao. Ninafikiri hawa watu wanatafuta sababu za kuchukizwa na nchi za kimagharibi.
Kuhusu dai kwamba ugonjwa umetokana na Mungu, ninaelewa kwamba mtu wa kidini angeweza kuliamini kwa sababu hawa wanaamini kwamba kila kitu kinafanywa duniani ni kwa kuwa ya Mungu. Lakini, sifikiri kwamba Mungu anaishi kwa hivyo siwezi kukubali kwamba ugonjwa huu ulitokana na Mungu.
Nakubali na Jason kwa sababu nafikiri pia kwamba Virusi vya Ukimwi unatokana na nyani badala ya wanasayansi wa kimagharibi. Nilisoma kuhusu awali ya Ukimwi na masomo yalisema ni kweli. Kwa kweli, watu wengi katika nchi ya Marekani, nchi ya kimagharibi, wana Ukimwi na wanakufa kama watu wengi katika nchi nyingi za Afrika. Kwa hivyo, wanasayansi wa kimagharibi hawataki kufa watu wao.
Kiangazi kilichopita nilifanya kazi kwa UNHCR kuhusu Virusi vya Ukimwi na wakimbizi na sikumbuki wakimbizi wananiambia kwamba walifikiri wanasayansi kutoka kimagharibi walitengeneza Virusi. Kwa kweli, waliniambia kwamba walifikiri Ukimwi ulitokana na nyani kama watu katika kimagharibi. Katika kazi yangu, nilijifunza watu wa DRC na hawafikiri wanasayansi wa kimagharibi wanajaribu kufa watu katika nchi za ulimwengu wa tatu. Wakati nyingi hawajui awali ya Ukimwi, lakini niliwafundisha.
Nilifundisha watu wengi katika Africa ya Mashariki kuhusu awali ya Ukimwi kwa sababu wanafunzi wangu walitaka kujua biologia ya Ukimwi, lakini abadani walifikiri watu kutoka kimagharibi wanajaribu kumaliza watu katika nchi za ulimwengu. Ikiwa ni kweli, kwa nini ningejaribu kufundisha njia ya kuishi na ukimwi na kuzuia Ukimwi? Nakubali Jason watu wanaofikiri ni wajinga sana. Ukimwi ni gonjwa baya sana na watu katika kila nchi wanahitaji kusaidia kuacha Ukimwi.
Nafurahi sana kusoma maoni yenu kufikia sasa. Ningependa tupate mchango wa Josiah na Clara ili tuendelee. Kila la heri.
Kama Jason, David, na Kate walisema nafikiri kwamba Ugonjwa wa Ukimwi umetokana na nyani. Lakini sijui kama sababu hiyo ni sababu nzuri zaidi yo yote. Inawezekana kwamba Ukimwi ni kutoka ugonjwa wa zamani. Katika wakati mrefu virusi hubadilisha ili hazitakuwa kutibiwa. Kwa mfano kuna magonjwa mengi yalioshindwa na dawa fulani. Lakini sasa dawa ile haiwezi kutibu magonjwa yale. Kwa hivyo, ninakubali na Jason kwamba labda Ukimwi umetokana na nyani, ingawa pia labda umetokana na virusi ya binadamu nyingine.
Kuhusu watu wanaosema kwamba ugonjwa huu ulitengenezwa na wanasayansi wa kimagharibi katika maabara, ninakubali na wanafunzi wengine tena. Kwa nini wanasayansi walitengeza ugonjwa huu ikiwa utawaua wenzangu wao, na pia ikiwa ugonjwa hautamwua mtu hadi miaka mingi (hata miaka mitano au kumi)? Watu wanaosema hiyo hawapendi nchi za kimagharibi kwa sababu sababu nyingine na sasa wanataka kuziaili nchi za kimagharibi.
Kuhusu kundi linaloshikilia kuwa Ukimwi ni adhabu kutoka kwa Mungu sijui kweli kama ninakubali. Ninaamini kwamba Mungu Anaweza kufanya kitu cho chote ambacho anapenda kufanya. Pia ninaamini kwamba Mungu ni mwadili na kama watu wanafanya vitu vibaya na dhambi Atawapa adhabu. Wakati mwingine Mungu Atatia adhabu hii kwa njia ya vitu ya Ulimwengu (kama magonjwa). Lakini sikuamini kwamba ni lazima kwamba Ukimwi ni adhabu ya Mungu, kwa sababu kuna vitu vibaya vingi ambavyo si adhabu ya Mungu bali ni kazi ya Shetani. Lakini watu wengi wanaosema hiyo wanataka chenga kuwabera watu wenye Ukimwi. Sikubali. Ninaamini kwamba njia ya mtu anataka kumfuata Mungu ni kutia huduma kwa wagonjwa. Kwa hivyo hatuwaberi watu wenye Ukimwi, bali tujaribu kuwasaidia.
Kuandika kifungu cha mwisho ni ngumu kwa sababu majibu ya wote ni sawa. Mimi ni mwanafunzi wa biologia, na pia nafikiri VVU ni dudu kama nyngi nyngine. Wanasayansi wametumia jinsi mbalimbali ya "gene sequencing" kusoma virusi vimetoka wapi. Masomo hawa yanadokeza kwamba virusi vya ukimwi vimetokana na nyani.
Kama Katelyn, nilikaa Afrika ya mashariki kufundisha watu kuhusu VVU na ugonjwa wa Ukimwi. Niliona haraka kwamba watu wengi walitaka kufahamu Ukimwi unatoka wapi. Kama amedhihirisha Mwalimu Mohochi, wachache walifikiri Ukimwi ulitengenezwa na wanasayansi wa Magharibi, wachache walifikiri ulitokana na nyani, na wachache waliamini ugonjwa huu ni adhabu kwa Mungu. Wakati wa kufundisha, sisi tulijaribu kueliza kwamba wanasayansi na wastadi wengi wanafikira VVU vinatokana na nyani. Halufu, lakini, tulisema ni kitu kidogo kufahamu sasa virusi vinatoka wapi kwa sababu ni tatizo kubwa katika kila nchi ya dunia. Sasa kitu kikuu ni kuelewa tunaweza kuviachaje na kufanya kazi pamoja kushinda Ukimwi.
Hii inashangaza kuona kuwa wanafunzi wanafundishwa upande mmoja. Mimi nilikaa afrika na ninaishi ulaya na america. Lakini ukisoma sayansi utaona kuwa Ukimwi umetengenezwa na wanasayansi. Habari ya nyani kutoka afrika ni sawa na habari ya zamani kuhusu afrika ina magonjwa kupiga vita watu, njaa watu hawakuli chakula, na mengineyo. Nimesoma kuhus Peter Duisberg yeye ni profesa hapa Berkely anasema kuhusu sayansi hii
watu wengi wananyamasisha wengine kusema ukimwi ulitoka wapi, kwasababu wao wanajua umetoka sayansi. Ni vizuri kusema, tutie bidii kuukomesha. lakini ni sawa pia kusema ulitoka wapi. Umesoma kuhusu Hepititis B waliokufa kule New York? Umesoma professors wengi wa Microbiology, na Cell biology na Molecular Biology wote wanasema ukimwi ni sayansi sio nyani. Afadhali kusema ukweli, na kutafuta njia ya kutibu. Bila kusema ukweli dunia haitapata madawa ya kweli kuhusu mwisho wa ukimwi.
Lakini watu wa misitu ya Afrika hawakuwa hapo juzi 1980? Walikuwa hapo miaka nyingi, na wao walikukula nyama ya nyani. Mnona hawakufa? Mbona hakukuja ukimwi?
ukisoma katika Lancet utaona wanasayansi walikosea kuhusu virusi ya simian. lakini habari hii haijulikani sana.
Ukimwi si kutoka Mungu, ni kutoka binadamu. labda sio kuua watu wa dunia ya tatu lakini serikali ya republican ilitaka kuua homosexual wa New York na San Franscisco
Niko pamoja na Mac Donald kuwa ugonjwa wa ukimwi umetengenezwa na wanasayansi kwa lengo la kuboresha na kukuza soko la dawa.
Niko pamoja na Mac Donald kuwa ugonjwa wa ukimwi umetengenezwa na wanasayansi kwa lengo la kuboresha na kukuza soko la dawa.
Post a Comment