Monday, May 26, 2008

Filamu

Habari zenu Wakenya wenzangu,
Wiki hii ningetaka kushughulika mada ya filamu kutokana na safari yetu ya kwenda kuona "Indiana Jones" jumapili jioni. Kwanza ningetaka kuwajua maoni yenu kuhusu filamu hii. Je unafikiri Steven Spielberg alifanya kazi nzuri katika uongozi wa filamu hii? Kulinganisha na filamu zake nyingine, filamu hii ilitokea vipi? Ungewanasihi rafiki zako kwenda kuangalia filamu hii au la? Kwa maoni yangu nilidhani kwamba filamu hii haikuwa nzuri sana na nilijipata nijiuliza mbona Speilberg hakuona maovu ya filamu hii.

Halafu ningetaka kuwauliza filamu ipi ndiyo unayopenda mno na kwanini? Nani maarufu aliigiza katika filamu hiyo na mhusika wake alikuwa na sifa zipi? Hatimaye, je umeshaangalia filamu nzuri ambayo inahusu Kenya? Filamu hiyo inaitwaje na ilikuwa ya kujisisimua?

Sunday, May 18, 2008

Uogeleaji

Maswali yangu ya leo yanasudiwa hasa kwa Jackson kwa sababu yanazingatia mambo ya uogeleaji lakini nafikiri kwamba pia Mohochi ataweza kuyajibu baadhi ya maswali. Wikendi hii Jason na mimi tumekuwa tukishindana katika mashindano ya uogeleaji pamoja na baadhi ya waogeleaji bora zaidi duniani na ningetaka kukuuliza Jason, je umefurahi na jinsi ambayo uliogelea katika mashindano haya? Mashindano haya yalikusaidiaje kujiandaa kwa mashindano ya Olympiki? Kuongeza, je utakuwa na mashindano mengine kabla ya kusafiri nchini Uchina? Ikiwa utakuwa na mashindano yo yote, hayo yatakuwa muhimu zaidi kuliko yale ya wikendi hii?

Aidha, tulifurahi sana kushangiliwa jumamosi kwa hivyo tunakushukuru mwalimu na sasa nina swali kwa wewe, ulijifunza nini katika mashindano ya wikendi na kuna kitu ambacho kilikushangaza? Na swali lingine ni kuhusu uhasimu. Kwa kawaida nchi za dunia ambazo zinapakana zina uhasimu mkali, Unafikiri ni tofauti katika Afrika Mashariki? Ninauliza swali hilo kwa sababu Yusufu alikuja na kupangaza bendera yake ya Tanzania lakini alikuwa akishangilia jirani yao ya Kenya. Hatimaye, Jason unafikiri kwamba mashangilio yanakusaidia kuogelea bora au unadhani kwamba hayana athari?

Monday, May 12, 2008

Chakula cha Taifa

Baada ya kuchoma na kula mbuzi wikendi hii iliyopita, ningetaka kuzingatia mada ya chakula, kwa wiki hii. Kuna vyakula vingi vya aina mbalimbali kote duniani, kwa hivyo ningetaka kuwauliza, je, ni chakula cha nchi ipi ambacho unakipenda mno na kwa nini? Mimi ninaipenda chakula cha nchi ya Thailand, hasa aina moja inayoitwa "Pad Thai," na inayojumuisha kamba, kuku na mboga ambao umechangyikwa katika tambi. Kweli ninfurahi nikiila!

Halafu ningetaka kuwaliza nyingi hujibu vipi mkiulizwa: Je, chakula cha taifa cha Kenya ni nini? Ninauliza swali hili kwa sababu mara nyingi sina jibu nzuri na mfupi.

Na hatimaye ningetaka kuwauliza: Iwapo unapatiwa fursa ya kula mlo mmoja na mtu mmoja maarufu, utachagua nani na utakula nini?

Sunday, May 4, 2008

Uchaguzi wa Urais wa Zimbabwe

Inaonekana kwamba matatizo yaliyoibuka kwa sababu ya uchaguzi wetu nchini Kenya yameanza kutulia kwa hivyo ningetaka tuhame nchini Zimbabwe ambapo shida zao zimekuwa zikiendelea kwa muda mrefu.
Wakati huu, kabla ya uchaguzi wa urais pamoja na ule wa bunge palikuwa na matumaini kuwa upinzani ungeshinda na juu ya hiyo kwamba kiongozi wa upinzani, Morgan Tsvangirai ungepata urais kutoka dikteta Mugabe. Ingawa ilikuwa wazi kuwa ZANU-PF ilijaribu kuiba kura kutoka upinzani hata hivyo MDC ilishika viti vingi zaidi katika uchaguzi wa bunge. Aidha, kitu sawa kilitokea katika uchaguzi wa urais, yaani Tsvangirai alipata kura nyingi kushinda Mugabe ingawa Mugabe aliiba kura nyingi. Lakini, kwa rasmi Tsvangirai hakupata asilimia ya kura ya kutosha ili awe rais (alipata asilimia arubaini na nane) na ZEC (Zimbabwe Electoral Commission) imenena kwamba Zimbabwe inapaswa kuwa na uchaguzi mwingine.
Tsvangirai mwenyewe anadai kwamba alishinda uchaguzi (na watu wote wanajua kwamba ni kweli) kwa hivyo hataki kuwa na uchaguzi tena, hasa kwa sababu anajua kwamba uchaguzi huu ufuatao hautakuwa wa haki. Lakini ikiwa hatasimama Mugabe atashinda urais. Kwa hviyo maswali yangu ni: Je, unafikiri kuwa Tsvangirai anapaswa kusimama katika uchaguzi ufuatao (re-run)? Au unadhani kwamba ni wakati ambao nchi za kimagharibi (au hata za Afrika) wanahitaji kuingilia mambo haya? Je, jinsi nzuri zaidi kusuluhisha matatizo ya Zimbabwe ni nini?

Monday, April 28, 2008

Matatizo ya chakula duniani

Kwa sababu tumeshaeleza mambo yaliyotokea katika safari yetu katika insha zetu, nilidhani kwamba ni mwafaka kuanzia mada tofauti. Ningetaka tuzungumzie matatizo yanayokabili dunia yetu kuhusu ukosefu na bei ghali za chakula, ambazo zinatatiza watu wengi kote duniani. Kila siku vyombo vya habari vinaripoti kuhusu maandamano yanayoendelea katika nchi kadha wa kadha kuhusu matatizo haya, na kwamba watu maskini milioni kadhaa hawawezi kujilisha. Kwa mfano, bei ya mchele, ambao ni chakula kikuu cha watu wengi duniani, imepandia asilimia tisini katika mwaka mmoja uliopita.

Nilisoma tu leo kuwa Katiba Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Ban Ki-Moon, baada ya mikutano anajitayarisha kutangaza mipango ya kujaribu kukabili shida zinazosababishwa na ongozeko la bei za chakula. Je, sababu zipi zimesababisha shida hii? Unafikiri mipango ambayo itatangazwa itasaidia vipi? Unadhani kuna sera ambazo zitaweza kufumbua (solve) matatizo haya na labda matatizo haya yametukia kwa upande kwa sababu hatuna uwezo wa kulisha idadi ya watu wanaoishi duniani leo?

Sunday, April 6, 2008

Kufuzu kwa Daudi Kwenda Olimpiki na Safari yenu ya Wingereza

Habari za leo? Nitaanza mfululizo wetu wa mada za blogu kwa muhula huu. Naanza kwa kumpongeza Daudi kwa dhati kwa kufaulu kujiunga na timu ya Kenya kwenda kwa michezo ya olimpiki mwaka huu. Pongezi.

Ningependa mkipata nafasi mtoe maelezo kuhusu safari yenu kwenda Wingereza pamoja na namna mashindano yenu yanavyoendelea. Aidha, nawatakia kila la heri huko.

Kwaherini.

Sunday, March 2, 2008

Amani katika nchi ya Kenya

Ninataka kurudi kuelekea mada ya juzijuzi kuhusu matukio baada ya uchaguzi wa rais wa Kenya wa mwaka uliopita. Sasa pande mbili za ODM na PNU wamekubailiana na viongozi wawili Raila na Kibaki wametia saina mkataba wa makubaliano. Ningetaka kuwauliza maoni yenu kuhusu siku za mbeleni kwa nchi yetu. Unafikiri kuwa ODM na PNU wataweza kujikaza vizuri baada ya kila kitu kimechofanyika?

Swali langu la pili ni kuhusu wale ambao wamefukuzwa nyumbani kwao au wale ambao wamepoteza familia na rafiki zao. Katika hotuba za viongozi, wote wawili walisisitiza kwamba sasa kitu muhimu sana cha kufanya ili kusonga mbele ni kusahau makabila na kuwasamehe wote kwa sababu wote ni wakenya. Je, ukipoteza kila kitu maishani kwako ungeweza kuwasamehe wale ambao walifanya hivyo kwako? Aidha, viongozi waliahidi kwamba watasaidia sana wale waliopotea nyumbani kwao, je unafikiri hii ni ahadi tupu?

Thursday, February 21, 2008

Rosa Mistika

Ningetaka kuanza mazungumzo mafupi kuhusu riwaya ya 'Rosa Mistika' tunayosoma wakati huu. Tumeona sifa za Rosa zikibadilika na tabia zake kuzorota na Kezilahabi anasema ni kwa sababu ya malezi yake. Je, katika maisha halisi unafikiri kwamba malezi yangeweza kusababisha sifa za mtu kubadilika upesiupesi kama jinsi sifa za Rosa zimebadilika? Je, kuhusu mbinu ya Padri kumzungumzia Rosa, ulifikiri mbinu zake zilikuwa mwafaka? Ungekuwa katika msimamo wake ungesema nini kujaribu kumsaidia Rosa? Unadhani kuna imani yo yote kwa Rosa?

Katika riwaya hii tunakabiliwa na swala la kutoa mimba na tunaona mawazo tofauti kuhusu swala hili. Je, maoni yako kuhusu swala hili ni nini? Unadhani mawazo ya Regina yangekuwa kuhusu swala hili yangekuwa tofauti iwapo angezaa wavulana tu?

Sunday, February 10, 2008

Mipango ya maisha yenu ya baadaye

Habari za leo?

Baada ya mjadala kuhusu hali ya kisiasa nchini Kenya pamoja na umuhimu na ongezeko la athari za Uchina ulimwenguni, nataka tugeukie swala tofauti linalohusiana na maisha yetu. Mimi napanga kurudi Kenya na kutoa mchango wamgu katika kufundisha. Aidha, nadhani nitafurahi mno ikiwa nitawza kuanzisha shule ya kuwasaidia vijana chipukizi kupata elimu nzuri. Tayari mimi nina mke na mtoto mmoja na napanga kupata wengine. Ningependa kujua mipango yenu ya baadaye maishani (baada ya Stanford). Zingatieni maswala kama masomo, kazi, familia, sehemu ya kuishi na kadhalika.

Monday, February 4, 2008

Mnataka mwe nini wakati ujao? (kutoka kwa Upendo)

Mnataka mwe nini wakati ujao?Hamjambo wote! Habari za wikendi? Nilifikiria kuhusu ninyi wikendi hii, na nilitanabahi nisijue nini mnataka mwe wakati ujao. Mimi, ningependa kuandika au kuumba sera ya afya kimataifa. Msiulize - sitaki kuwa dakta. Ningependa kuwa mwanasheria ambaye anajua mambo mengi kuhusu sheria ya dunia na ya haki za watu. Kwa hivyo, nilisoma historia mpaka mwaka huu, na sasa, ninasoma elimu jamii (hasa kuhusu siasa linganishi) ili nifahamu hali ya dunia nzima.Na nyi? Mnataka kuwa nini wakati ujao? Na kwa nini?Tutaonana kesho! ~Upendo

Saturday, January 26, 2008

Umuhimu wa Uchina

Ingawa mauaji yanaendelea katika nchi yetu na hawajasuluhisha cho chote, nilifikiri kuwa nitatoa mazungumzo yetu kwa mkondo na kuwauliza maswali machache kuhusu Uchina. Juzi katika chajio nilikuwa nikzungumza na rafiki zangu kuhusu lugha za Uchina na umuhimu wao. Kulikuwa na wale ambao walinena kwamba katika siku za usoni itakuwa muhimu zaidi kuelewa lugha hizo kwa sababu angalau asilimia ishirni ya umma wa dunia wanatoka Uchina. Kwa hivyo swali langu ni: Je, unadhani kwamba ni muhimu kujifunza lugha hizo hata usipotaki kwenda kuishi nchini Uchina?

Swala langu la pili ni kuhusu upanuzi wa Uchina. Uchumi wake umekuwa ukikua kwa miaka thelathini tangu serikali iliongoa shughuli za nchi. Kuna sababu nyingi kuhusu maendeleo ya uchumi wake lakini watu hutaja kwamba Wachina hawajali haki za binadamu na kwa hivyo wanaweza kufanya cho chote ili watengeneze pesa. Mfano maarufu ya hii ni kuwa Uchina wanashirikiana kwa shingo upande mjini Darfur. Kwa hivyo, swali langu ni: Je, unafikiri kwamba nchi za kimagharibi wana haki za kujiingiliza shughuli za Wachina ili wasimamishe matukano ya haki za binadamu yanayoendelea nchini Uchina na aidha katika sehemu nyingine duniani? Kulikuwa wazo la kugoma olympiki mwaka huu kwa sababu ya dhima ya Uchina nchini Sudan, unadhani kwamba wazo lingebadilisha kitu?

Friday, January 18, 2008

Maandamano nchini Kenya

Wiki ningetaka kuendelea na mazungumzo yetu ya wiki iliyopita kuhusu matatizo yanayoendelea Kenya. Kwa siku tatu sasa, washabiki wa wapinzani wamekuwa wakiandamana dhidi ya matokeo ya uchaguzi baada ya matangazo ya viongozi wa ODM wiki iliyopita kufanya hivyo. Taarifa za habari zimeripoti kwamba watu zaidi ya kumi wameuawa na wengi wameshtaki polisi kwa vitendo yao. Kwa hivyo swali langu la kwanza ni je, unadhani kwamba polisi wamefanya kazi mbaya wakijaribu kusimamisha maandamano? Ikiwa hawangejiingiliza (interfere), hali ingekuwa heri kuilko sasa?

Juu ya hayo, Annan yuko karibu kufika Kenya kwa ziara yake na atazungumza na Raila na Kibaki ili ajaribu kupata amani. Iwapo ungekuwa Annan ungewaambiaje viongozi hawa? Mpango wako kujaribu kutafuta suluhisho ili Kenya irudie hali ya kawaida ungekuwa nini?

Hatimaye, wapinzani wametangaza watagoma (boycott) mashirika mbalimbali yanayommilikiwa na wenza Wakikuyu wa Kibaki. Je unadhani kwamba kitendo hiki kitakuwa na manufaa kuhusu utafutaji wa suluhisho?

Saturday, January 12, 2008

Uchaguzi wa Urais Nchini Kenya

Habari za wikendi?

Hali iliyoibuka nchini Kenya baada ya uchaguzi wa mwezi jana ilikuwa kinyume kabisa na matarajio ya watu wengi. Kwa maoni yako, hali hii inaweza kuwa na athari gani kwa taifa? Je, unadhani ingeweza kuepukika? Hatua gani zaweza kuchukuliwa kutoa suluhisho?

Jioni njema.