Thursday, February 21, 2008

Rosa Mistika

Ningetaka kuanza mazungumzo mafupi kuhusu riwaya ya 'Rosa Mistika' tunayosoma wakati huu. Tumeona sifa za Rosa zikibadilika na tabia zake kuzorota na Kezilahabi anasema ni kwa sababu ya malezi yake. Je, katika maisha halisi unafikiri kwamba malezi yangeweza kusababisha sifa za mtu kubadilika upesiupesi kama jinsi sifa za Rosa zimebadilika? Je, kuhusu mbinu ya Padri kumzungumzia Rosa, ulifikiri mbinu zake zilikuwa mwafaka? Ungekuwa katika msimamo wake ungesema nini kujaribu kumsaidia Rosa? Unadhani kuna imani yo yote kwa Rosa?

Katika riwaya hii tunakabiliwa na swala la kutoa mimba na tunaona mawazo tofauti kuhusu swala hili. Je, maoni yako kuhusu swala hili ni nini? Unadhani mawazo ya Regina yangekuwa kuhusu swala hili yangekuwa tofauti iwapo angezaa wavulana tu?

4 comments:

Daudi said...

Kwanza ningetaka kupongeza Jackson kuhusu hiari yake ya mada hii- riwaya hii inaanza kunifurahisha sana njama inapopanua kwa hivyo ninafurahi kuzungumza maudhui ya ‘Rosa Mistika.’ Kweli, sifa za Rosa zimebadilika sana. Katika miaka miwili amebadilika, kutoka kuwa msichana mnyamavu amabaye hakupenda kushirikiana na wavulana, kwa kuwa msichana ambaye huhonya na hajali athari za matendo yake. Ninadhani kwamba katika maisha halisi mabadaliko hayo yanaweza kusababishwa na malezi fulani kana yale ya Rosa kwa hivyo msimamo wangu ni sawa na ule wa mwandishi. Kezilahabi anatumia tashbihi mzuri kueleza sababu za watoto kubadilika wanapopewa uhuru kutoka wazazi wao. Mwandishi anaandika kuwa mti ukinyima mwanga wa kutosha kwa awali, hatimaye utajaribu kupita miti yote ili upate mwanga. Ninafikiri tashbihi hii ni mwafaka katika maisha halisi. Ingawa bila shaka kuna wale ambao wamelelewa kwa jinsi sawa ya Rosa wanaoendelea kuishi vizuri baada ya kuondoka nyumbani, kuna wengine wanaotaka kuvunja minyororo amabyo imewekwa na wazazi wao.

Kuhusu swala la Padri, ni wazi kwamba alijitahidi lakini ni ngumu sana kusaidia mtu ambaye hataki kusaidiwa au ambaye hadhani kwamba anahitaji msaada. Nikiwa katika viatu vyake sijui kama ningelitendea kwa jinsi tofauti, bila shaka ningelihamaki kwa sababu Rosa alikosa heshima na hakutaka kusikia kitu cho chote. Lakini, kwa maoni yangu bado kuna imani kwa Rosa. Akifukuza ukaidi wake ataweza kubadailisha sifa zake tena.

Kweli, Jackson umefungua swala kubwa sana ya ulimwengu wa sasa kuhusu kutoa mimba. Ninadhani kwamba kama msichana si tayari kulelea mtoto ni bora zaidi kutoa mimba kwa sababu mtoto ambaye halelewi vizuri ana nafasi kubwa zaidi kuwa mtu mbaya kuliko wao wanaolelewa vizuri. Aidha, pengine si kosa la mwanamke mwenyewe kuwa na mimba. Nafikiri wanawake ambao wamenajisiwa wanapaswa kuwa na hiari ya kutoa mimba. Hatimaye, sidhani kwamba Regina angekuwa na mawazo tofauti kuhusu kutoa mimba angezaa wavulana tu. Ninafikiri kwamba anahisi vibaya kwa rafiki yake Bigeyo na kwa sababu hawezi kuzaa mtoto Regina hapendi kuwaona wengine wakitoa mimba. Aidha katika jamii nyingi watu hawaridhia yo yote mambo ya kutoa mimba.

mohochi said...

Mimi naendelea kufurahishwa sana na michango yenu.

Katika jamii za kiafrika, watoto walichukuliwa kuwa baraka kubwa kutoka kwa Mungu (ingawa wengine awali hawakumuamini Mungu wa kidini za kisasa). Aidha, ndio walikuwa mali ya pekee waliyoithamini zaidi watu. Katiki misingi hiyo, watoto walipendwa sana. Mtu asiyekuwa na mtoto alijihisi kuwa mpungufu. Kwa sababu hiyo hakuna aliyetaka kukosa watoto. Jambo la kutoa mimba halikuwepo. Kwa kweli hadi sasa wazee wengi hawaelewi kabisa kwa nini mtu atoe mimba. Haikujalisha kama mtoto ni wa kiume au la-wote walipaswa kuongeza furaha kwa wazazi wao. Hata hivyo, ni kweli pia kwamba jamii nyingi zilithamini zaidi watoto wa kiume. Nadhani Regina bado angepinga utoaji wa mimba hata kama tayari angekuwa na watoto wengi wa kiume. Kwa sbabu ya imani yangu ya kidini, siungi mkono utoaji mimba lakini, binafsi, nadhani ni vibaya kuwataka waliobakwa pamoja na wale ambao wanahatarisha afya zao kuendelea kuibeba mimba hadi mwisho wake.

somal said...

kuto ridhika na watoto wa jinsi moja ni tatizo ambalo wanalo waafrika walio wengi. hawalidhiki wakiwa na watoto wa kiume tu au kuwa na watoto wa kike tu. mama regina asingeridhika hivyohivyo kama angekuwa na watoto wengi wakiume. angehitaji awe na watoto wa kike tena. nalengo la kufanya hivyo huwa ni kumlidhisha mwanamme hata kama hana mawazo hayo, ingawawengine huwa ni msukumo kwa wanawake kutafuta watoto wa jinzia tofauti.

juu ya rosa kuwa alivyo ni kweli malezi yamechangia kwa kiasi kikubwa. wazazi wake walitumia nguvu sana katika kuzuia matendo yake maovu badala ya kumuelimisha madhala ya kuwa na mahusiano na ya kimapenzi katika umri mdogo. hivyo alivyokuja kuibukia ukubwani akawa hana elimu ya kjilinda na madhara yatokanayo na mapenzi na asiweze kushaulika tena. wazazi tukumbuke, SAMAKI MKUNJE ANGALI MBICHI, lakini mkunje taratibu asidhurike.

Unknown said...

mtoto asipofunzwa na mamake hufunzwa na ulimwengu. hii ni kusema kuwa hali changanyifu inayomkumba Rosa ni kutokana na kifungo cha kufuli cha wazazi wake hasa Zackaria. kuhusu jsmbo ls Padri, hakuna lolote ambalo angeweza kufanya kwakuwa alikuta maji yashamwagika na hivyo hayawezi kuzoleka. hivyo \padri angemshawishi polepole mpaka apate tunda; la sivyo, matokeo kaangalia.