Ninataka kurudi kuelekea mada ya juzijuzi kuhusu matukio baada ya uchaguzi wa rais wa Kenya wa mwaka uliopita. Sasa pande mbili za ODM na PNU wamekubailiana na viongozi wawili Raila na Kibaki wametia saina mkataba wa makubaliano. Ningetaka kuwauliza maoni yenu kuhusu siku za mbeleni kwa nchi yetu. Unafikiri kuwa ODM na PNU wataweza kujikaza vizuri baada ya kila kitu kimechofanyika?
Swali langu la pili ni kuhusu wale ambao wamefukuzwa nyumbani kwao au wale ambao wamepoteza familia na rafiki zao. Katika hotuba za viongozi, wote wawili walisisitiza kwamba sasa kitu muhimu sana cha kufanya ili kusonga mbele ni kusahau makabila na kuwasamehe wote kwa sababu wote ni wakenya. Je, ukipoteza kila kitu maishani kwako ungeweza kuwasamehe wale ambao walifanya hivyo kwako? Aidha, viongozi waliahidi kwamba watasaidia sana wale waliopotea nyumbani kwao, je unafikiri hii ni ahadi tupu?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
Nadhani kwamba kama wananchi wengi wa Kenya, nina wasiwasi mwingi kuhusu siku za usoni za nchi yetu. Itakuwa vigumu sana kwa baadhi ya wanasiasa katika PNU na wengine katika ODM kuafikiana baada kila kitu kilichofanyika baada ya uchaguzi. Nina imani kubwa kwamba wataweka hali wa Kenya mbele ya wao wenyewe na kuona kwamba kwa kazi kuendelea katika Kenya wanapaswa kushirikiana. Nadhani kwamba kuna wanasiasa ambao wanaona haja za kushirkiana lakini ninaogofia wale ambao wanaonyesha kwamba hawajali maisha ya wananchi; wanataka mabenzi manne tu! Lakini, hata nikiwa na wasiwasi nimefurahi kwamba viongozi wetu wametia saini kwa sababu ni hatua ya kwanza ya kurudishia Kenya kwenye barabara ya maendeleo.
Kuhusu swali la pili, ninaamini itakuwa vigumu sana kwa watu kusameheana baada ya mgogoro uliotukia miezi iliyopita. Lakini licha ya ugomvi, Wakenya ni maarufu kote duniani kwa sababu ya uwezo wao kuweka tofauti zao kando na kuendelea kusaidiana. Wakiongozwa mwafaka na wakipewa msaada wa kujenga tena maisha yao, nafikiri uhusiano baina ya makabila mbalimbali utaimarisha. Nafikiri wakati tu utatuelezea maelekeza yapi yatachukuliwa na nchi yetu.
Hatimaye kuhusu swali la tatu, kama ni kawaida kwa viongozi wetu, ahadi hizi zinaonekana kana kwamba ni ahadi tupu. Kibaki bado anafikiri kila kitu kilichofanyika ni mzaha na siamini kwamba kweli ataweza kushirikiana na Raila vizuri. Raila anaonekana kama anawaza maswala yanayokabili Kenya vizuri kuliko Kibaki na atajitahidi zaidi kusaidia wananchi bali nina wasiwasi kwamba atakomeshwa na mayai mabaya katika PNU. Kwa jumla, kwa sababu wao ni wanasiasa, kwa kweli ni vigumu kuamua maneno gani yanayosemwa yana maana halisi. Ningetaka kuamini kwamba watafuata maneno yao na matendo lakini historia imetuonyesha mara nyingi kwamba yale yanayoahdiwa na viongozi wetu hayatokei.
Post a Comment