Friday, January 18, 2008

Maandamano nchini Kenya

Wiki ningetaka kuendelea na mazungumzo yetu ya wiki iliyopita kuhusu matatizo yanayoendelea Kenya. Kwa siku tatu sasa, washabiki wa wapinzani wamekuwa wakiandamana dhidi ya matokeo ya uchaguzi baada ya matangazo ya viongozi wa ODM wiki iliyopita kufanya hivyo. Taarifa za habari zimeripoti kwamba watu zaidi ya kumi wameuawa na wengi wameshtaki polisi kwa vitendo yao. Kwa hivyo swali langu la kwanza ni je, unadhani kwamba polisi wamefanya kazi mbaya wakijaribu kusimamisha maandamano? Ikiwa hawangejiingiliza (interfere), hali ingekuwa heri kuilko sasa?

Juu ya hayo, Annan yuko karibu kufika Kenya kwa ziara yake na atazungumza na Raila na Kibaki ili ajaribu kupata amani. Iwapo ungekuwa Annan ungewaambiaje viongozi hawa? Mpango wako kujaribu kutafuta suluhisho ili Kenya irudie hali ya kawaida ungekuwa nini?

Hatimaye, wapinzani wametangaza watagoma (boycott) mashirika mbalimbali yanayommilikiwa na wenza Wakikuyu wa Kibaki. Je unadhani kwamba kitendo hiki kitakuwa na manufaa kuhusu utafutaji wa suluhisho?

3 comments:

Daudi said...

Kwanza ningetaka kusema kuwa nimefurahi kwamba umechagua kuendelea na mada hii kwa sababu ninafikiri kwamba wakati huu ni muhimu sana kwa nchi yetu na kila uamuzi ambao viongozi wanafanya unaweza kuathiri nchi yote.

Mambo yanaendelea kutukia baina ya washabiki wa upinzani na polisi yamenihuzunisha kabisa kwa sababu ninadhani kwamba polisi wamefanya kazi mbaya sana. Labda si kosa la polisi wenyewe lakini la viongozi wao ambao wamewaamuru polisi kutumia risasi za halisi dhidi watu amabao hawana silaha, hiyo ni upuzi tu. Kwanza, ninadhani kwamba watu wanapaswa kuwa na haki ya kuandamana hasa dhidi kitu kinacho umuhimu zaidi kama uchaguzi wa mwezi wa jana. Kwa hivyo dhima ya polisi inapaswa kuwa kuthibitisha kuwa watu wanaoandama hawavunji vitu, polisi hawapaswi kupigana na wao. Halafu, kuna njia tofauti kusimamisha maandamo badala ya kuwaua watu. Polisi wanaweza kusimamisha maandamano na rizazi za plastiki, mitambo ya moto na kadhalika, kwa njia hii labda watu wataumia kidogo lakini hawatakufa. Sasa, watu wamekasirika zaidi na polisi na serikali kwa sababu ya mauaji kwa hivyo mzunguko katili utaendelea.

Wiki ijayo nilinena kwamba matatizo ya nchi yatasuluhishwa ikiwa tuwe na uchaguzi tena lakini wakati huu kuwa na wachungaji kutoka ng’ambo kuhakikisha kwamba uchaguzi ni wa haki. Kwa hivyo, nikiwa Annan ningewaambia Kibaki kwamba akijalia nchi yake hata kidogo anapaswa kubali kuwa na uchaguzi tena. Wakati huu, raia wamepoteza heshima ya viongozi wao na watu hawaamini kwamba rais wetu ni rais wa kweli. Hakuna matarajio katika nchi ikiwa watu hawana imani kwa viongozi.

Sina matumaini kuwa mgomo utakuwa na athari. Kwanza Kibaki ameshaonyesha kwamba hajali kuhusu wenzake kwa hivyo mgomo hutabadilisha maoni yake. Aidha, kweli sidhani kwamba watu wanaweza kugoma vifaa vya Wakikuyu. Kwa mfano watu watasafiriaje bila matatu? Watakunywa maziwa yapi bila Brookside? na kadhalika.

Kwa hivyo, kila moja wenu anasubiri kwa matarajio kwamba Kibaki atafukuza ukaidi wake na mazungumzo baina Annan, Raila na yeye yatafanikiwa lakini bila ushirika wa Kibaki hatutakuwa karibu zaidi kupata suluhisho ya matatizo haya.

Daudi said...
This comment has been removed by the author.
mohochi said...

Habari za sasa? Mimi vile vile nafurahi kuona kuwa tumeendeleza mada hii muhimu. Jambo linalonisikitisha zaidi ni matamko ya watu wengine "serikalini"(mbali na Kibaki). Wanachofanya ni kuonyesha kiburi ambacho hakitatupeleka mbali. Itakuwa vizuri mno iwapo Kibaki mwenyewe atajitokeza na kushiriki kikamilifu badala ya kuwaachia Michuki, Kalonzo, Karua, Mutua na wenzao kupayuka ovyo.

Nafurahi kuona kuwa leo Kibaki na Raila wamekutana kwa mara ya kwanza. Nisingependa kuzungumza sana kuhusu kilichotokea mwezi jana, lakini nadhani ni muhimu zaidi kwa sasa kuzungumza na kusimamisha mauaji yanayoendelea. Natumai kuwa hayo yatawezekana. Ningekuwa Annan ningewambia wahusika wazi wazi kuwa nchi ya Kenya pamoja na wananchi wake ni muhimu kuliko tamaa zao.

Naungana na Daudi kusema kuwa polisi, japo wana wajibu wa kulinda nchi, wanapaswa kutekeleza wajibu huo kwa njia mwafaka na zinazokubalika kimataifa. Sidhani kuwa kuwapiga watu risasi ni moja kati ya njia hizo.

Kwa maoni yangu njia bora zaidi ni kuunda serikali ya mpito ikijumuisha pande zote mbili, na kuipa muda wa miaka miwili kuishughulikia katiba ya Kenya. Baada ya hapo, tufanye uchaguzi mwingine kwani tukiwa na katiba nzuri haitajalisha sana rais ni nani.

Mungu aibariki Kenya. Daudi sasa ni wakati wako kuchangia mada.