Kwa sababu tumeshaeleza mambo yaliyotokea katika safari yetu katika insha zetu, nilidhani kwamba ni mwafaka kuanzia mada tofauti. Ningetaka tuzungumzie matatizo yanayokabili dunia yetu kuhusu ukosefu na bei ghali za chakula, ambazo zinatatiza watu wengi kote duniani. Kila siku vyombo vya habari vinaripoti kuhusu maandamano yanayoendelea katika nchi kadha wa kadha kuhusu matatizo haya, na kwamba watu maskini milioni kadhaa hawawezi kujilisha. Kwa mfano, bei ya mchele, ambao ni chakula kikuu cha watu wengi duniani, imepandia asilimia tisini katika mwaka mmoja uliopita.
Nilisoma tu leo kuwa Katiba Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Ban Ki-Moon, baada ya mikutano anajitayarisha kutangaza mipango ya kujaribu kukabili shida zinazosababishwa na ongozeko la bei za chakula. Je, sababu zipi zimesababisha shida hii? Unafikiri mipango ambayo itatangazwa itasaidia vipi? Unadhani kuna sera ambazo zitaweza kufumbua (solve) matatizo haya na labda matatizo haya yametukia kwa upande kwa sababu hatuna uwezo wa kulisha idadi ya watu wanaoishi duniani leo?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
3 comments:
Ni kweli kwamba dunia yenye matatizo makubwa mengi kuhusu ukosefu na bei ghali za chakula. Kuna sababu kadhaa zinazosababisha shida hizi. Kwanza, watu wengi ni maskini kiasi cha kwamba hawawezi kununua cho chote kula na sasa kwa sababu ya bei za vyakula zimepanda kuna watu wengi kuliko zamani katika nafasi hiyo. Kwa hivyo wao wanategemea Mradi wa Chakula wa Dunia (WFP) kujilisha lakini shirika hilo halina pesa ya kutosha kuwalisha watu wote ambao wanahitaji chakula. Lakini katika mipango ya Bw. Ban Ki-Moon, WFP imenena kwamba inataka kutafuta dolar milioni mia saba hamsini na tano ili kuwalisha. Kwa hivyo nadhani kwamba WFP ikifaulu kupata pesa hizo itaweza kusaidia watu wengi lakini itakuwa suluhisho kwa wakati huu tu.
Kusuluhisha matatizo haya vitu vingi vinapaswa kubadilishwa. Kwanza, serikali za kimagharibi zinahitaji kusimamisha kuwapatia wakulima wao pesa ili waweze kuuza mazao yao kwa bei chini kidogo katika nchi zao. Mambo haya yanazuia wakulima wa nchi za ulimwengu wa tatu kuuza mazao yao ng'ambo kwa sababu hawawezi kushindana na bei hizo. Kwa hivyo, soko la chakula duniani likiwa huru na wakulima wa kila kote wakiweza kufanya biashara na nchi zo zote, wakulima maskini wengi wangesaidiwa sana. Halafu wakulima hawa wangeweza kusaidia wananchi wao ambao wanakosa chakula. Tatizo lingine ambalo linapaswa kurekebishwa ni mambo ya nchi za kimagharibi ya kutouza vyakula vyao ng’ambo ili kuzilinda akiba za chakula. Haya yanasababisha bei za chakula kupanda sana na hayo ni mojawapo tatizo kuu wakati huu.
Bila shaka, ninafikiri kwamba idadi ya watu amabao wanaishi duniani ni tatizo kubwa lakini hiyo ni kitu ambacho hatuwezi badilisha wakati huu. Kwa hivyo ili kusaidia wao watu ambao hawawezi kujilisha vitu ambavyo vinaweza kubadilishwa vinahitaji kubadilishwa upesi.
Asante sana Jason kwa kuanzisha mada hii. Nakubaliana nawe kuwa haingekuwa mwafaka kuendelea na mada ile kwani mlikuwa mmeishughulikia tayari katika insha zenu.
Maswali yako ni ya kimsingi mno. Daudi ametoa maelezo mazuri sana kuhusu hali ya nchi za kimagharibi kuwalipa wakulima wao ili bei ya mazao yao iwe ya chini. Ingawa kwa kufanya hivyo wanaathiri ulimwengu mzima, si wana haki kuhakikisha kuwa wakulima wao wametosheka na wanaendelea kulima? Ni kwa nini nchi zinazoendelea hazifanyi mikakati bora ya kuendeleza kilimo? Nafikiri kuwa hata nchi maskini zina hatia ya kuwapuuza wakulima ambao ni uti wa mgongo wa chumi za nchi zao. Tumewapuuza wakulima na kupuuza kilimo kiasi kuwa wakulima wanajidharau na kujichukia. Watu wasiokuwa na elimu ya kutosha kupata kazi mijini ndio wanageukia kilimo kwa sababu ya uhitaji bali si kwa sababu wanapenda kuwa wakulima. Aidha, katika baadhi ya nchi, wakulima huwekeza pesa nyingi zaidi ya mapato yao baada ya kuuza mazao yao. Matokeo yake ni kuwa wanageukia shughuli nyingine.
Umoja wa mataifa unapaswa kuandaa sera nzuri za kuzisaidia nchi maskini kujenga hali ya kujitosheleza katika utoaji wa chakula. Bila hilo, haitakuwa rahisi kukusanya pesa za kutosha kuwalisha watu wote walio na uhitaji wa chakula.
Post a Comment