Saturday, January 12, 2008

Uchaguzi wa Urais Nchini Kenya

Habari za wikendi?

Hali iliyoibuka nchini Kenya baada ya uchaguzi wa mwezi jana ilikuwa kinyume kabisa na matarajio ya watu wengi. Kwa maoni yako, hali hii inaweza kuwa na athari gani kwa taifa? Je, unadhani ingeweza kuepukika? Hatua gani zaweza kuchukuliwa kutoa suluhisho?

Jioni njema.

3 comments:

Daudi said...

Kwanza, ningetaka kunena huzuni yangu kuhusu uchaguzi wetu wa rais wa mwaka jana. Kabla ya uchaguzi, ilikuwa dhahiri kuwa wananchi wa Kenya walikuwa wamechoshwa na serikali ya PNU na ufisadi ambao ulikuwa ukiendelea, kwa hivyo ilionekana kwamba kiongozi wa upinzani, Raila Odinga, atashinda uchaguzi. Isipokuwa Wakikuyu, waliowengi wa Kenya walimpigia kura Raila kwa matarajio kwamba uchaguzi ungekuwa uaminifu lakini kwa bahati mbaya Kibaki aliamua kwamba alitaka kujiunga orodha ndefu ya viongozi wa Afika ambao hawataki kujitoa urais.

Tumeshaona kwamba uamuzi wa PNU kupemba maraia wa Kenya umekuwa na athari baya sana. Watu wengi wameuawa na wengine wamekosa nyumbani kwao kwa sababu ya mapigano. Lakini si wao tu ambao wameteseka, kila mkenya ataathiriwa na ukaidi wa Kibaki na makuu yake. Kampuni za kimagharibi watakopesha fedha kwa riba kwa shingo upande kwa nchi yetu na aidha watali hawatataka kutembelea nchi ya Kenya kwa muda mrefu sasa. Hivi vitu viwili vitaathiri uchumi wetu ambao umekuwa ukikua kwa muda, kwa hivyo biashara kwa nchi yote itaanza kupotewa na uzuri.

Lakini, nadhani kwamba kuna nafasi ya kubadilisha kila kitu Kibaki akianza kufikiria wananchi wake. Kitu bora zaidi cha kufanya kingekuwa kufanya uchaguzi tena lakini wakati huu kuwa na wachunga kutoka ng’ambo. Ikiwa tuna uchaguzi uaminifu, nadhani kwamba hali ya nchi itarudishwa kuwa nzuri. Kwa mkono mwingine, sina matarajio makubwa kwamba Kibaki na PNU wanataka kufumbua tatizo la sasa kwa sababu ameshakataa pendekezo la upinzani kuwa na uchaguzi mwingine na pia kukataa msaada wa rais wa Ghana, John Kufuor.

Kwa huzuni inaonekana kama Mwai Kibaki hataki kusaidia nchi yetu na isipokuwa mtu anaweza kubadilisha maoni yake, Kenya itakuwa na matatizo makubwa.

Jason said...

Swala la uchaguzi uliotukia mwezi uliopita linanihuzunisha sana kwa sababu mimi ninabudu nchi yangu na kuona hali ya maisha ikiharibika nchini Kenya kunasababisha uchungu moyoni mwangu. Tayari, kwa sababu ya hali iliyotokea baada ya uchaguzi, watu zaidi ya mia sita wameuawa na laki kadhaa wamekuwa wakimibizi. Maisha ya watu wengi yameharibiwa: nyumba zao zimechomwa, biashara zao zimebomolewa, hawana chakula au pesa ya kutosha na watoto wao hawana uwezo wa kurudi shuleni. Aidha, biashara na makampuni makubwa kwa mfano makampuni ya chai yameathiriwa vibaya. Wafanyakazi wao bado hawana njia rahisi ya kuenda kazini kwa sababu usafirishaji wa umma hasa katika maeneo ya magharibi umeathiriwa. Aidha, makampuni mengi yameteseka kwa sababu bidhaa nyingi zimekwama bandarini Mombasa na nilisoma kwamba meli zilikuwa zikiondoka bila kushusha bidhaa zao kwa sababu bandari ya Mombasa imeshindwa na idadi ya bidhaa katika wakati huu. Uchumi wa Kenya, na hata wa nchi nyingine za Afrika Mashariki, unateseka vibaya kwa sababu ya mambo hayo kwa sababu upande mkubwa wa uchumi huu unategemea makampuni ambayo yanapaswa kutumia bandari ili waweze kuingiza bidhaa yanazohitaji na kupeleka vitu vyao ugaibuni.

Juu ya hayo, hali hii nchini Kenya tayari imeathiri na itaendelea kuathiri utali vibaya sana, ambao utaathiri uchumi zaidi kwa sababu sana sana Kenya inategemea fedha za ng’ambo, zinazoletwa na watali. Niliongea na babangu jana na amesema kwamba biashara yake ya hoteli inafanya kazi kwa asilimia ishirini ya kawaida na inaendelea kuwa mbaya zaidi. Wakenya wengi wanaajiriwa katika sehemu ya utali kwa hivyo watathiriwa vibaya iwapo wengi wao watapoteza kazi zao kwa sababu ya utovu wa watali.

Kwa maoni yangu, hali ingeweza kuepukika ikiwa Bw. Odinga angekuwa rais wetu. Siku mbili baada ya uchaguzi nadhani kwamba wananchi wa Kenya walikuwa wamepokea Odinga kama rais mpya kwa sababu chama cha ODM kilikuwa kimeshinda wingi wa viti bungeni. Nchi yote ilishtuka Bw. Kibaki alipotangazwa kama mshindi wa uchaguzi na hata baada ya tangazo lake, Bw. Kivuitu, mwenyekiti wa ECK, alisema kuwa hakujua mshindi mkweli katika uchaguzi, lakini bado alitangaza matokeo ambayo kwa wazi yalikuwa na ila nyingi. Ni vigumu kutolaumu Waluo na washabiki wengine wa Odinga kwa hasira yao na ilikuwa hasira hii ambayo ilisababisha ghasia na vifo vya watu mia sita na ambayo inasababisha matatizo ya nchi yetu.

Sidhani kwamba kuna suluhisho rahisi ya matatizo haya yanayosababishwa na uchaguzi wa mwezi uliopita. Suluhisho moja ingekuwa Kibaki apatie Odinga urais au kuunda serikali ya mseto pamoja naye na kufanya uchaguzi mwingine huru na nafuu. Hata hivyo sidhani kuwa wanacnchi watakuja katika idadi za mara ya kwanza kwa sababu siasa imewachosha sana.
Lakini sasa nafikiri ni wazi kwamba Kibaki hataki mazungumzo na wapinzani na hafanyi cho chote cha maana kujaribu kuponya nchi yetu. Kweli hali ya nchi yetu si nzuri na nina wasiwasi nyingi ya siku za usoni. Tunaomba Mungu kuwa viongozi wetu wazungumze na Kibaki aanze kujali matatizo ya raia wa Kenya ambayo yamesababishwa na ujinga wake, ili nchi irekebishwe na wananchi waanze kujenga tena maisha yao.

mohochi said...

Daudi na Jason, hongereni kwa mchango mzuri kuihusu mada hii. Ama kwa kweli mimi sina la kuongeza kwani mmeyaweka bayana matatizo ambayo yamejitokeza pamoja na kupendekeza njia za kuyatatua. Kulingana na habari ambazo nimezipata hivi punde, Keneth Marende, mbunge wa chama cha ODM, ameshinda kura na kuteuliwa kama spika wa bunge. Sijui hili litamaanisha nini katika harakati za kutafuta suluhisho la mzozo wa kisiasa uliopo nchini Kenya. Na tuwe na subira tuone.