Sunday, April 29, 2007

Uchaguo Katika Marekani

Kwa sababu mimi ni mwanafunzi wa Uhisano wa Kimataifa, ningependa kuanza mazungumzo kuhusu siasi hapa Marekani. Baada ya kuandika kuhusu uchanguo unaokuja, nitaeleza maswali kuhusu Uchaguo wa Rais was Marekani Katika Miaka Mia Mbili na Nane. Ningependa kujua maoni ya wanafunzi katika darasa hili kuhusu watajaji kwa ofisi kwa wingi wa kushoto au "democrats."

Kwa wingi wa kushoto, watajaji wawili wakubwa ni Barack Obama na Hillary Clinton. Hillary ni mzungu tu lakini Barack (jina hili lina maana ya "blessed" katika Kiswahili) ni Mswahili nusu. Babake alizaliwa na aliisha katika Kenya na mamake alitoka jimbo la Kansas katika Marekani. Kila mtajaji alizaliwa katika Marekani kwa sababu ni uhitaji kukimbia kwa Rais wa Marekani.

Uchaguo hawa utakuwa muhimu sana kwa sababu kwa kawaida Rais wa Marekani ni mzungu na mwanaume, kwa sababu Hillary ni mwanamke na Barack ni Marekani Mwafrika. Ina maana ya ikiwa wingi wa kushoto inashinda uchaguo, kwa wakati wa kwanza katika historia ya Marekani, kutakuwa rais wa mwanamke au rais wa mweusi. Ni kitu kikubwa kabisa kwa sababu kisogoni cha Marekani kulikuwa kirahi sana dhidi ya watu wa mweusi kwanza na baadaye kirahi sana dhidi ya wanawake. Je, unafikiri mtajaji yupi atashinda uchaguo wa msingi wa wingi wa kushoto na kwa nini? Pia, nani atakuwa Rais wa Marekani katika miaka mia mbili na nane, mtu wa wingi wa kushoto au mtu wa wingi wa kulia? Unafikiri watu wa Marekani wanahitaji badilisho katika kiongozi wa serakali? Kwa nini?

6 comments:

Jason said...

Sasa swala hili ni gumu. Si rahisi kuagua nani atashinda uchaguzi wa mrengo wa kushoto lakini kwa maoni yangu nadhani kuwa Obama atashinda. Obama ni mtu mverevu zaidi na pia anaelewa matatizo ya watu mbalimbali kuliko Hilary. Pia, wakati Marekani ilipokuwa ikiamua kuruka mpaka kwenda Iraq, Obama alikuwa akipinga uamuzi huu, lakini Hilary alikubali Rais Bush na wenzake. Kwa hivyo tofauti hii inaonyesha kwamba Obama ana nguvu na akili nyingi kuliko Hilary na ataweza kuongoza nchi hii vizuri zaidi bila kuathiriwa na wengine. Aidha ninadhani kuwa ni wakati wa Mwafrika kuongoza nchi hii na kuathiri ulimwengu.

Katika uchaguzi wa rais wa Marekani wa mwaka wa 2008 ninafikiri mrengo wa kushoto utashinda kwa sababu wananchi wa Marekani wamechoka na mambo ya mrengo wa kulia. Wanataka vita vya Iraq vimalizwe, na wanajeshi waje nyumbani. Bush alidanganja wananchi wa Marekani kuhusu silhaa ya kinuklia nchini Iraq kwa hivyo watachukia mrengo wa kulia katika uchaguzi. Mrengo wa kushoto wameshinda tayari wingi wa viti vya Nyumba kwa hivyo nadhani kwamba ni wakati wao kushinda urais.

Binafsi, ninaona kuwa maisha hapa Marekani yanahitaji mabadiliko ya uongozi hasa kaitka urais, kwa sababu maelekezo ya siasa yameharibika. Wanasiasa wa mrengo wa kulia wanapenda vita na wana matatizo mengi nchini Iraq. Obama akishinda urais, ninajua ataweza kupeleka nchi hii mbele na kufaulu katika ulimwengu wa kisasa. Pia, kwa sababu ana damu ya Mkenya ni lazima awe na moyo mkubwa kama simba kwa hivyo atakuwa na uongozi waminifu na imara.

Daudi said...

Ninaafikiana na Jason na ninafikiri kwamba Obama atashinda uchaguzi wa mrengo wa kushoto. Hata sijui vingi kuhusu siasa ya Marekani lakini ninadhani kuwa Obama anapendwa kuliko Hilary. Aidha, nakubaliana na Jason kwamba Obama anaelewa matatizo ya watu wengi kuilko Hilary.

Ninadhani kuwa mrengo wa kushoto atashinda kwa sababu watu wengi wanachukizwa na Bush na wamechoka na vita vya Iraq. Lakini, kwa maoni yangu ingekuwa heri ikiwa mrengo wa kulia kushinda.

Lakini, kama nilieleza sijui mengi kuhusu siasa ya Marekani. Kwa hivyo, ingawa ningependelea mrengo wa kulia kushinda, nafikiri kuwa Obama angekuwa rais mzuri kwa sababu mwenye akili. Katika Afrika Mashariki watu husema "akili ni mali" kwa hivyo Obama akiwa kiongozi, Marekani itakuwa na mali zaidi.

mohochi said...
This comment has been removed by the author.
mohochi said...

Naam, tuendelee hivyo jamani. Nani atachangia mada itakayofuata hii ya Kate?

Claire said...

Ni ngumu kuagua nani atashinda michujoni ya wingi wa kushoto kwa sababu maneno machache mabaya au mazuri yanaweza kubadilisha vitu vyote katika kitambo kifupi. Ninafikiri Obama na Clinton wote wawili ni watajaji waguvu. Wawili wana akili, lakini wote pia wangehitaji kupiga kondo kali kufika urais.

Katika nchi hii, watu wengi hawana akili fumbuka. Wao watachagua Raiz kulingana na anatukiaje rudingani, na siyo anasemaje. Pia watu hawa wanaogopa mabadiliko. Wataogopa kweli kuchagua mtajaji mweusi au mwanamke (alipokuwa hawana sababu nzuri). Kuna tatizo lingine ambalo linaonyesha vizuri "double standard" linaloishi Marekani. Obama atakuwa na shida kwa sababu ni kijana, na watu watasema kwamba hajapata uzoefu. Hillary ni mzee kuliko Obama, lakini kwa sababu yeye ni mwanamke watu hawatapendi umri wake. Watu hutetea zaidi wanamke vijana ambao wamekoa hata hawana uzoefu kabisa.

Mimi ninajua nchi hii inahitaji badiliko kubwa katika serikali. Vitu vikiendelea hivyo, vitahakikisha kwamba nchi hii itajiharibika na nchi zingine pia.

Joe said...

Kama marafiki yangu waliosema swala hili ni gumu. Ninakubali na Claire kwamba itakuwa vigumu sana kwa Obama au Hillary kushinda uchaguzi kwa sababu Obama ni mtajaji mweusi na Hillary ni mwanawake. Sifikiri kwamba hii ni sababu nzuri lakini katika Marekani, hasa kusini ya nchi ya Marekani sababu hii ni kweli. Obama atakuwa na shida kwa sababu yeye ni kijana na hawana uzoefu. Lakini pia Hillary ana shida kwa sababu yeye ni wanawake na anaandamana na mumu wake Bill Clinton. Nitafikiri kwamba Hillary atashinda Obama lakini sifikiri atashinda uchaguzi kwa nchi yote.

Maoni yangu ni kwamba ninapenda mrengo wa kulia zaidi, na ningependa mtu kutoka mrengo huu ashinde lakini sijui nani atashinda. Uchaguzi huu ni nafasi bora zaidi kwa Hillary au Obama kujaribu kuwa rais kwa sababu Jason alisema watu wenji hawapendi mrengo wa kulia sana. Lakini labda ile itabadilisha kabla ya Uchaguzi. Nani anajua?