Saturday, January 26, 2008

Umuhimu wa Uchina

Ingawa mauaji yanaendelea katika nchi yetu na hawajasuluhisha cho chote, nilifikiri kuwa nitatoa mazungumzo yetu kwa mkondo na kuwauliza maswali machache kuhusu Uchina. Juzi katika chajio nilikuwa nikzungumza na rafiki zangu kuhusu lugha za Uchina na umuhimu wao. Kulikuwa na wale ambao walinena kwamba katika siku za usoni itakuwa muhimu zaidi kuelewa lugha hizo kwa sababu angalau asilimia ishirni ya umma wa dunia wanatoka Uchina. Kwa hivyo swali langu ni: Je, unadhani kwamba ni muhimu kujifunza lugha hizo hata usipotaki kwenda kuishi nchini Uchina?

Swala langu la pili ni kuhusu upanuzi wa Uchina. Uchumi wake umekuwa ukikua kwa miaka thelathini tangu serikali iliongoa shughuli za nchi. Kuna sababu nyingi kuhusu maendeleo ya uchumi wake lakini watu hutaja kwamba Wachina hawajali haki za binadamu na kwa hivyo wanaweza kufanya cho chote ili watengeneze pesa. Mfano maarufu ya hii ni kuwa Uchina wanashirikiana kwa shingo upande mjini Darfur. Kwa hivyo, swali langu ni: Je, unafikiri kwamba nchi za kimagharibi wana haki za kujiingiliza shughuli za Wachina ili wasimamishe matukano ya haki za binadamu yanayoendelea nchini Uchina na aidha katika sehemu nyingine duniani? Kulikuwa wazo la kugoma olympiki mwaka huu kwa sababu ya dhima ya Uchina nchini Sudan, unadhani kwamba wazo lingebadilisha kitu?

1 comment:

Jason said...

Nashukuru Daudi kwa maswali yako. Kwa sadfa wiki iliyopita, hata mimi nilikuwa nikizungumzia mada ya athari ya Uchina duniani na umuhimu wa kujifunza lugha yao ya Mandarin. Kwa maoni yangu ninafikiri kwamba umuhimu wa kujifunza lugha hii unategemea malengo yako katika maisha yako. Nadhani kwamba ukitaka kuingia dunia ya biashara, uwezo wa kusema lugha ya Mandarin kidogo itaendelea kuwa muhimu kwa sababu ya upesi wa maendeleo ya uchumi wa Uchina. Uchina unashirikishwa katika maagano mengi ya biashara kote dunia kwa sababu ya haja yake ya raslimali ili uendeleze maendeleo ya uchumi wake na ujipatiaji wa fedha ya kigeni.

Kwa habari ya swali lako la pili, ninadhani kwamba nchi za kimagharibi zina haki kubwa ya kujiingiliza shughuli za Wachina zikiona kwamba Uchina unatukana haki za binadamu. Kwa sababu sasa Uchina umeimarika kuwa mojawapo ya nchi zinazoongoza dunia yetu na una athari nyingi kote dunia, una wajibu wa kutoa mfano mzuri kwa nchi nyingine hasa za ulimwengu wa tatu. Kwa hivyo ikiwa Uchina hutoi mfano mzuri na hujali haki za binadamu, nchi za kimagharibi zina wajibu wa kutenda. Lakini licha ya mahitaji ya nchi za kimagharibi kushinikiza Uchina kupokea wajibu wao wa kutetea haki za binadam, sidhani kuwa wazo la kususia Olimpiki lingefaa wo wote. Kwa miaka mingi serikali imekuwa ikifanyia nchi yake tayari ili mpango wa Michezo ya Olimpiki ufanikiwe nchini mule. Kwa hiyo uamuzi wa nchi za kimagharibi kutoenda kushindana ungetatiza sana uhusiano baina ya nchi hizi na Uchina. Haya matatizo yangeleta shida nyingi duniani kwa hivyo nchi za kimagharibi zinapaswa kutafuta njia nyingine ya kushawishi Uchina kupokea wajibu wake wa kuheshimu haki za binadam.