Sunday, April 29, 2007

Uchaguo Katika Marekani

Kwa sababu mimi ni mwanafunzi wa Uhisano wa Kimataifa, ningependa kuanza mazungumzo kuhusu siasi hapa Marekani. Baada ya kuandika kuhusu uchanguo unaokuja, nitaeleza maswali kuhusu Uchaguo wa Rais was Marekani Katika Miaka Mia Mbili na Nane. Ningependa kujua maoni ya wanafunzi katika darasa hili kuhusu watajaji kwa ofisi kwa wingi wa kushoto au "democrats."

Kwa wingi wa kushoto, watajaji wawili wakubwa ni Barack Obama na Hillary Clinton. Hillary ni mzungu tu lakini Barack (jina hili lina maana ya "blessed" katika Kiswahili) ni Mswahili nusu. Babake alizaliwa na aliisha katika Kenya na mamake alitoka jimbo la Kansas katika Marekani. Kila mtajaji alizaliwa katika Marekani kwa sababu ni uhitaji kukimbia kwa Rais wa Marekani.

Uchaguo hawa utakuwa muhimu sana kwa sababu kwa kawaida Rais wa Marekani ni mzungu na mwanaume, kwa sababu Hillary ni mwanamke na Barack ni Marekani Mwafrika. Ina maana ya ikiwa wingi wa kushoto inashinda uchaguo, kwa wakati wa kwanza katika historia ya Marekani, kutakuwa rais wa mwanamke au rais wa mweusi. Ni kitu kikubwa kabisa kwa sababu kisogoni cha Marekani kulikuwa kirahi sana dhidi ya watu wa mweusi kwanza na baadaye kirahi sana dhidi ya wanawake. Je, unafikiri mtajaji yupi atashinda uchaguo wa msingi wa wingi wa kushoto na kwa nini? Pia, nani atakuwa Rais wa Marekani katika miaka mia mbili na nane, mtu wa wingi wa kushoto au mtu wa wingi wa kulia? Unafikiri watu wa Marekani wanahitaji badilisho katika kiongozi wa serakali? Kwa nini?

Tuesday, April 24, 2007

Upimaji wa Dawa

Utaratibu kuunda dawa kutibu Ukimwi ni urefu na tatizo sana. Makampuni ya dawa kwa kawaida yanatoka Marekani au Ulaya wa Magharibi. Ili inawezekana makampuni ya dawa yauze dawa yao, kwanza inahitaji kupita majaribio mengi. Majaribio ya kwanza hufanyika na seli halafu na wanyama. Kama haya yanaendelea vizuri, dawa yanawezekana kujaribiwa katika binadamu. Ili upate matokeo mazuri katika muda mfupi, makampuni yanataka kufanya marajibio ya binadamu katika Waafrika kwa sababu watu wengi wana Ukimwi.

Pia, matokeo yanafanyika haraka zaidi inapotumiwa "placebo" kulinganisha na dawa mpya (badala ya dawa ambayo imeshatumiwa kutibu wagonjwa). Kawaida hii haingeruhusiwa katika Marekani ama Ulaya, lakini wanasayansi wanasema kwamba kwa sababu la Waafrika wengi hawawezi kupata tibu kwa kawaida, ni nzuri zaidi kwamba angalau nusu watapata dawa katika jaribio. Kuhusu nusu wengine, hawatakipoteza kitu chochote.

Wengine wanasema kwamba kutumia 'placebos' ni sawa kwa sababu itahimiza maendeleo ya dawa, halafu dawa mpya itapatikana mapema zaidi kwa matumizi ya wagonjwa. Je, mnafikiri ni ya maadili (ethical) zaidi kutumia placebos au kuwakimu dawa nyngine (the "basic minimum of care" inapatikana katika Marekani au sehemu za Afrika) watu wa kundi ya kulinganisha?

Friday, April 13, 2007

Mada ya Ardhi

Tafadhali msome kifungu kifuatacho:

Wawili wauawa Uganda
(Kutoka tovuti ya BBC 12/04/07)

Polisi nchini Uganda wameelezea kwamba watu wawili wameuawa katika mji mkuu wa nchi hiyo, Kampala, wakati wa maandamano ya kupinga mipango ya serikali ya kutaka kuugawa msitu mmoja nchini humo kwa familia moja yenye asili ya ki-Asia.
Polisi walifyatua risasi za kuwashambulia baadhi ya wa-Asia walioonekana.
Serikali ya nchi hiyo imekuwa ikipendekeza kuubadilisha msitu huo na kuwa kiwanda cha sukari, kwa kuugawa msitu huo kwa kampuni ya sukari nchini Uganda.
Kampuni hiyo imesema itatoa ajira nyingi na kusaidia kipato cha wananchi wa Uganda lakini wanamazingira wanasema mradi huo unaweza kusababisha kumomonyoka kwa ardhi.


Ardhi ya umma ianaleta vigambo vikubwa katika Afrika Mashariki kwa sababu baadhi ya watu hasa matajiri wanataka kuitumia ardhi kwa mashamba au kujenga majengo makubwa ya ofisi na nyumba. Je, unadhani ni muhimu zaidi kukinga mazingira au kufanya miradi ili nchi iweze kuharakisha maendeleo ya uchumi? Kwa nini unadhani wananchi wengi wa Uganda hawataki kiwanda cha sukari ambacho kingeleta ajira? Nani ana haki kuamua jinsi ardhi itumike, serikali au wananchi?

Friday, April 6, 2007

Chanzo cha UKIMWI

Kumekuwa na mjadala wa muda mrefu sana kuhusu chanzo cha ugonjwa wa Ukimwi (Aids). Wapo wanaosema kuwa ugonjwa huu ulitengenezwa na wanasayansi wa kimagharibi katika maabara ili kupunguza idadi ya watu katika nchi za ulimwengu wa tatu. Wengine wanasema kuwa ugonjwa huu umetokana na nyani. Aidha, kundi lingine linashikilia kuwa Ukimwi ni adhabu kutoka kwa Mungu kwa sababu watu wamekuwa wabaya na watenda dhambi. Wewe una maoni gani kuhusu jambo hili, na kwa nini?