Inaonekana kwamba matatizo yaliyoibuka kwa sababu ya uchaguzi wetu nchini Kenya yameanza kutulia kwa hivyo ningetaka tuhame nchini Zimbabwe ambapo shida zao zimekuwa zikiendelea kwa muda mrefu.
Wakati huu, kabla ya uchaguzi wa urais pamoja na ule wa bunge palikuwa na matumaini kuwa upinzani ungeshinda na juu ya hiyo kwamba kiongozi wa upinzani, Morgan Tsvangirai ungepata urais kutoka dikteta Mugabe. Ingawa ilikuwa wazi kuwa ZANU-PF ilijaribu kuiba kura kutoka upinzani hata hivyo MDC ilishika viti vingi zaidi katika uchaguzi wa bunge. Aidha, kitu sawa kilitokea katika uchaguzi wa urais, yaani Tsvangirai alipata kura nyingi kushinda Mugabe ingawa Mugabe aliiba kura nyingi. Lakini, kwa rasmi Tsvangirai hakupata asilimia ya kura ya kutosha ili awe rais (alipata asilimia arubaini na nane) na ZEC (Zimbabwe Electoral Commission) imenena kwamba Zimbabwe inapaswa kuwa na uchaguzi mwingine.
Tsvangirai mwenyewe anadai kwamba alishinda uchaguzi (na watu wote wanajua kwamba ni kweli) kwa hivyo hataki kuwa na uchaguzi tena, hasa kwa sababu anajua kwamba uchaguzi huu ufuatao hautakuwa wa haki. Lakini ikiwa hatasimama Mugabe atashinda urais. Kwa hviyo maswali yangu ni: Je, unafikiri kuwa Tsvangirai anapaswa kusimama katika uchaguzi ufuatao (re-run)? Au unadhani kwamba ni wakati ambao nchi za kimagharibi (au hata za Afrika) wanahitaji kuingilia mambo haya? Je, jinsi nzuri zaidi kusuluhisha matatizo ya Zimbabwe ni nini?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
Maoni yangu ni kwamba nchi za ulimwengu walipaswa kuingilia mambo ya Zimbabawe zamani yalipokuwa yakianza kuzorota na sijui ni nini wanangojea. Wameweka vikwazo lakini ni wazi kwamba vikwazo hivi havijaathiri Mugabe hata, na ni wananchi ambao wanateseka. Naamini kwamba jeshi linapaswa kutumwa Zimbabawe kuondoa Mugabe.
Tsvangirai hana budi ya kusimama tena kwa sababu ya masiala ya katiba ambayo Daudi ameshaeleza. Kwa hivyo kufikia sasa sioni njia ambayo anaweza kupata urais bila msaada kutoka ugaibuni.
Kwa sasa sidhani kwamba ye yote ameona suluhisho ya mambo haya mbali na Mugabe na wenzake ambao wanaona mipango yao ikianza kufaulu.
Post a Comment