Tuesday, October 30, 2007

Kumkaribisha Emily na kujitambulisha

Karibu sana Emily katika mawasiliano yetu haya. Ni furaha yetu kuwa nawe katika blogu ya Kiswahili. Aidha, asante kwa kujitambulisha kwetu. Naamini kwamba washiriki wengine nao watajitambulisha ili ujue unawasiliana na nani (mimi naamini wote mwanijua).

Hongera kwa uchaguzi wenye amani na utulivu. Je, waweza kusema machache kuhusu serekali ya wanafunzi hapo chuoni? Kwa mfano, inajumuisha viongozi wangapi na majukumu yao ya kimsingi ni nini? Wanayatekeleza vizuri? Siasa za ukabila zinajitokeza ndani yake au la? Hatimaye kwa nini wewe hukugombea nafasi yoyote? Baadaye, tutatarajia wanafuzni wa hapa Stanford kutueleza kama kuna mfumo kama huo huku.

Usiku mwema.

Sunday, October 21, 2007

Wikendi

Wikendi hii, nimeshughulika sana kwa sababu nimehitaji kufanya kazi zangu za chuo na vile vile timu yetu ya uogeleaji imekuwa na kurutu katika wikendi yote. Aidha, tulikuwa na mazoezi ya uogelaji jumamosi asubuhi na yalifuatwa na finali ya kombe cha dunia cha ragbi ambacho Afrika Kusini ilishinda.
Kwahivyo, jumamosi baada ya mazoezi, chamshakinywa na mchezo wa ragbi, nilienda kucheza 'frisbee' pamoja na timu na kurutu. 'Frisbee' ni mchezo ambao watu wanatupana diski inayoweza kuruka mbali sana. Baada ya mchezo huu, sisi wote tulienda nje kula katika mkahawa wa Meksiko. Baada ya chajio, tena pamoja tukaenda kucheza mchezo mwingine amabo katika kiingereza unaitwa 'bowling.' Katika mchezo huu, unahitaji kutupa mpira mgumu ili uangushe mingi ya miti kumi unayoweza.
Lakini, usiku wa jumamosi, baada ya kucheza 'bowling,' nilianza kuhisi vibaya, kwa hivyo niliamua kulala mapema wengine walipokuwa wakisherekea.
Sasa, asubuhi ya jumapili, ninahisi bora kuliko jana usiku lakini nina kazi nyingi ya kuandika kabla ya mwisho wa wikendi.