Sunday, May 18, 2008

Uogeleaji

Maswali yangu ya leo yanasudiwa hasa kwa Jackson kwa sababu yanazingatia mambo ya uogeleaji lakini nafikiri kwamba pia Mohochi ataweza kuyajibu baadhi ya maswali. Wikendi hii Jason na mimi tumekuwa tukishindana katika mashindano ya uogeleaji pamoja na baadhi ya waogeleaji bora zaidi duniani na ningetaka kukuuliza Jason, je umefurahi na jinsi ambayo uliogelea katika mashindano haya? Mashindano haya yalikusaidiaje kujiandaa kwa mashindano ya Olympiki? Kuongeza, je utakuwa na mashindano mengine kabla ya kusafiri nchini Uchina? Ikiwa utakuwa na mashindano yo yote, hayo yatakuwa muhimu zaidi kuliko yale ya wikendi hii?

Aidha, tulifurahi sana kushangiliwa jumamosi kwa hivyo tunakushukuru mwalimu na sasa nina swali kwa wewe, ulijifunza nini katika mashindano ya wikendi na kuna kitu ambacho kilikushangaza? Na swali lingine ni kuhusu uhasimu. Kwa kawaida nchi za dunia ambazo zinapakana zina uhasimu mkali, Unafikiri ni tofauti katika Afrika Mashariki? Ninauliza swali hilo kwa sababu Yusufu alikuja na kupangaza bendera yake ya Tanzania lakini alikuwa akishangilia jirani yao ya Kenya. Hatimaye, Jason unafikiri kwamba mashangilio yanakusaidia kuogelea bora au unadhani kwamba hayana athari?

1 comment:

Jason said...

Ningetaka kutoa shukrani kubwa kwa maswali yako Daudi, kwa sababu kweli mada ya uogeleaji ni kitu ambacho ninakipenda kuzungumzia sana. Kujibu swali lako la kwanza, nilifurahi na baadhi ya mbio zangu lakini si zote. Kwa mfano nilitaraji kwamba nitaogelea upesi jioni katika fainali, lakini katika kila mbio niliogelea taratibu zaidi. Sijui shida ilikuwa nini, lakini ni kitu ambacho nitapaswa kurekebisha kabla ya Olimpiki. Licha ya hayo, katika mbio yangu ya kujifurahisha mno ambayo ni mita mia moja kipepeo, niliogelea muda wa sekudi hamsini na tatu nukta arobaini, ambao ulinifurahisha sana kwa sababu ni muda wangu nzuri mno katika mazoezi magumu. Kwa hivyo ninatarajia kwamba nitaweza kupunguza wakati wangu mzuri mno wa sekundi hamsini nukta themanini na tano nikifika Beijing baada ya kupumzika zaidi.

Mashindano haya yalinisadia kujiandaa kwenda Olimpiki kwa sababu yalinipatia fursa ya kufanya mazoezi ya mbio zangu dhidi ya waogeleaji hodari ambao wengine watakuwa wakielekea Beijing pia. Nilijifunza vitu vingi katika mbio zangu ambavyo nitapaswa kuimarisha, kwa mfano jinsi ninayozunguka ukutani. Vitu hivi vitarekebishwa na mazoezi mengine. Aidha niliogelea mara kumi katika siku tatu, bali mjini Beijing nitakuwa nikiogelea mara sita kwa upeo katika siku saba. Kwa hivyo mashindano haya yalinipatia mazoezi mazuri.

Kabla ya Olimpiki nitakuwa nikielekea mjini LA tarehe sita ya mwezi wa sita kushindana katika "Janet Evans Invitational," na tena nadhani kwamba waogeleaji wazuri watukuwepo. Halafu nina mpango wa kwenda nchini Kanada kushindana katika mashindano mjini Winnipeg katika mwezi wa saba. Timu ya uogeleaji ya Olimpiki ya Kanada itakuwepo, na waogeleaji hawa watanipatia ushindani mzuri. Mashindano haya yatakuwa muhimu katika kiwango cha sawa na wikendi hii iliyopita kwa sababu yataniruhusu kujiandaa vizuri tena.

Hatimaye Daudi, swali lako la mwisho lina jibu la wazi ambalo ni bila shaka mashangilio ya rafiki zangu yananisaidia sana kuogelea bora zaidi, hasa kama washabiki hawa ni wananchi wa Afrika Mashariki! Mashangilio hayo yananisababisha kuhisi hisia za uzalendo ambazo zinazidisha nguvu yangu. Kwa hivyo ningetaka kuchukua fursa hii kushukuru sana Mohochi, Yusufu na George kwa kuja Jumamosi kutushangilia- kweli ina maana nyingi kwetu. Asanteni sana.