Habari zenu Wakenya wenzangu,
Wiki hii ningetaka kushughulika mada ya filamu kutokana na safari yetu ya kwenda kuona "Indiana Jones" jumapili jioni. Kwanza ningetaka kuwajua maoni yenu kuhusu filamu hii. Je unafikiri Steven Spielberg alifanya kazi nzuri katika uongozi wa filamu hii? Kulinganisha na filamu zake nyingine, filamu hii ilitokea vipi? Ungewanasihi rafiki zako kwenda kuangalia filamu hii au la? Kwa maoni yangu nilidhani kwamba filamu hii haikuwa nzuri sana na nilijipata nijiuliza mbona Speilberg hakuona maovu ya filamu hii.
Halafu ningetaka kuwauliza filamu ipi ndiyo unayopenda mno na kwanini? Nani maarufu aliigiza katika filamu hiyo na mhusika wake alikuwa na sifa zipi? Hatimaye, je umeshaangalia filamu nzuri ambayo inahusu Kenya? Filamu hiyo inaitwaje na ilikuwa ya kujisisimua?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
2 comments:
Ninafurahi kuzungumzia safari yetu ya kuiangilia filamu ya “Indiana Jones.” Kweli ninapenda kubarizi na mwalimu wetu pamoja na Yusufu, na kwenda kuangilia filamu kulikuwa fursa mwafaka kufanya hiyo lakini. Lakini kama Jackson nilidhani kwamba filamu hii haikuwa nzuri sana hasa kulinganisha na filamu nyingine za Spielberg au hata zile za zamani kuhusu “Indiana Jones.” Katika uongonzi wa filamu wake, nafikiri kwamba Spielberg alifanya kazi nzuri akiongoza “Schindler’s List” ambayo ni filamu kuhusu mauaji ya Wayahudi katika Vita Vya Dunia Vya Pili. Aidha, nilipenda filamu yake kuhusu papa aitwayo ‘”Jaws.” Mimi mwenyewe singehimiza mtu kuenda kuangilia filamu mpya ya ‘Indiana Jones’ lakini ni wazi kwamba watu wanaipenda, kwa hivyo nadhani kwamba ni bora kuacha watu kuona filamu wenyewe na kuunda maoni yao.
Kuhusu swali lako lingine, filamu ninayopenda zaidi inaitwa “Shawshank Redmption.” Filamu hiyo ilitungwa katika miaka ya tisini na inahusu mwanabenki (banker) ambaye alishtakiwa kwa kumwua mkewe. Ingawa mume huyu hakumwua mkewe alifungwa gerezani kwa maisha yake yote. Muda mrefu wa filamu unapitwa ndani ya gereza na ploti inafuata matokeo yake mbalmbali. Hatimaye kuna mwisho wa kufurahisha lakini sitaki kuuharibu kwa watu ambao hawajaiona filamu hiyo, kwa hivyo sitawaambia nini inatokea mwishoni.
Kuhusu swala la filamu zinazohusu Kenya. Nimesikia kwamba filamu aitwayo “Out of Africa” ni filamu nzuri lakini sijawaji kuiona. Lakini filamu ambayo ilinisisimua na mandhari yake ni katika Kenya, inaitwa “To Walk With Lions.” Filamu hiyo inahusu maisha ya George Adamson ambaye alijikaza kulinda simba katika mbunga ya wanyama ya Kora.
Kwa hivyo, ingawa filamu ya “Indiana Jones” haikunisisimua zaidi, safari tuliyofanya ilinistarehesha.
Mimi si mfuasi mzuri wa maswala ya filamu lakini tutazungumza darasan leo.
Post a Comment