Baada ya kuchoma na kula mbuzi wikendi hii iliyopita, ningetaka kuzingatia mada ya chakula, kwa wiki hii. Kuna vyakula vingi vya aina mbalimbali kote duniani, kwa hivyo ningetaka kuwauliza, je, ni chakula cha nchi ipi ambacho unakipenda mno na kwa nini? Mimi ninaipenda chakula cha nchi ya Thailand, hasa aina moja inayoitwa "Pad Thai," na inayojumuisha kamba, kuku na mboga ambao umechangyikwa katika tambi. Kweli ninfurahi nikiila!
Halafu ningetaka kuwaliza nyingi hujibu vipi mkiulizwa: Je, chakula cha taifa cha Kenya ni nini? Ninauliza swali hili kwa sababu mara nyingi sina jibu nzuri na mfupi.
Na hatimaye ningetaka kuwauliza: Iwapo unapatiwa fursa ya kula mlo mmoja na mtu mmoja maarufu, utachagua nani na utakula nini?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
Asante Jackson, nimefurahi kuondoka kutoka kuzungumza kuhusu siasa na matatizo duniani na kuelekea mada ambayo wote wanipenda yaani chakula. Kweli, napenda kula vyakula vya aina mbalimbali lakini ningepaswa kusema kwamba aina ninayopenda sana ni vyakula kutoka nchi ya Japan. Pale nchini Japan wanakula aina za samaki mbichi nyingi na aidha wanyama wengine wa bahari wakimeo pueza, kamba ndogo, kamba, kaa na kadhalika. Aina ya vyakula hii inaitwa ‘sushi’ na pengine chakula kibichi kinaandaaliwa na wali. Kwa hivyo, ingawa ninapenda aina ya vyakula vingi, ladha ya ‘sushi’ inanisisimua zaidi.
Kujibu swali lako linalofuata, nafikiri kwa sababu ya makabila mengi ya Kenya ambayo yana vyakula vyao vya kienyeji ni gumu kuamua vile ambavyo ni vya taifa na vile ambavyo ni vya kabila tu. Lakini, nadhani kwamba ‘Ugali na sukumawiki’ inafuzu kuwa chakula cha taifa cha Kenya.
Hatimaye, ningeweza kuchagua mtu ye yote duniani na kula naye ningechagua Robert Mugabe (laiti hataniua) kwa sababu ningetaka kujua sababu zake za kuharibu nchi hiyo na kutesa watu wao. Labda atanionyesha upande mwingine kuhusu dhambi yake yote. Katika mlo ule, tungekula ‘sushi’ kwa sababu ni chakula ambacho ninapenda sana lakini nadhani kwamba kingemtesa.
Post a Comment