Sunday, March 2, 2008

Amani katika nchi ya Kenya

Ninataka kurudi kuelekea mada ya juzijuzi kuhusu matukio baada ya uchaguzi wa rais wa Kenya wa mwaka uliopita. Sasa pande mbili za ODM na PNU wamekubailiana na viongozi wawili Raila na Kibaki wametia saina mkataba wa makubaliano. Ningetaka kuwauliza maoni yenu kuhusu siku za mbeleni kwa nchi yetu. Unafikiri kuwa ODM na PNU wataweza kujikaza vizuri baada ya kila kitu kimechofanyika?

Swali langu la pili ni kuhusu wale ambao wamefukuzwa nyumbani kwao au wale ambao wamepoteza familia na rafiki zao. Katika hotuba za viongozi, wote wawili walisisitiza kwamba sasa kitu muhimu sana cha kufanya ili kusonga mbele ni kusahau makabila na kuwasamehe wote kwa sababu wote ni wakenya. Je, ukipoteza kila kitu maishani kwako ungeweza kuwasamehe wale ambao walifanya hivyo kwako? Aidha, viongozi waliahidi kwamba watasaidia sana wale waliopotea nyumbani kwao, je unafikiri hii ni ahadi tupu?