Tuesday, June 19, 2007

Likizo yangu ya Kiangazi 2007

19/06/07

Leo ni leo. Niliamka kwenda kuogelea mapema na nilifanya vizuri sana licha ya mwili wangu ambao umekamatwa na mafua. Baada ya mazoezi, nilirudi chumba changu kulala kidogo lakini usingizi wangu ulikuwa mkubwa kwa hivyo nilikaa kitandani kwa masaa manne! Hatimaye nilipoamka, niliandaa chakula cha mchana na nilikikula na rafiki yangu. Sasa ninaketi kwa kompyuta nikifanya mazoezi ya hii lugha safi na ninasikitika darasa letu la mwaka uliopita. Tafadhali muandike vitu vichache kueleza safari zenu!